logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Iyanii aingia "uchi " kwenye hafla ya Arrow Bwoy

Iyanii aliwashangaza mashabiki baada ya kuingia uchi katika uzinduzi wa album ya Arrow Bwoy.

image
na Radio Jambo

Burudani14 March 2022 - 10:08

Muhtasari


• Msanii Iyanii aliwashangaza mashabiki baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa album ya Arrow Bwoy akiwa uchi.

• Aliwataka mashabiki wake kukubali kwamba muziki ni sanaa na kwamba msanii lazima afanye mambo yasiyo ya kawaida ili kuzidi kutamba.

Instagram, KWA HISANI

Msanii Iyanii aliwashangaza mashabiki baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa album ya Arrow Bwoy akiwa uchi.

Akizungumza kwenye mahojiano na mwanablogu Mungai Eve, Iyanii alisema kwamba vazi hilo [chupi na karatasi ya nailoni] lilimgharimu zaidi ya shilingi laki moja.

Iyanii alisema alichagua vazi hilo kwa kuwa yeye ni msanii ambaye analenga matao ya kimataifa kwa hivyo lazima hatua yoyote anayopiga iwe na ukali wa aina yake.

Aliongeza kwamba alinunua vazi hilo kutoka taifa ya Ufaransa.

Aidha mwanamuziki huyo alisema kwamba hakufanya hivo ili kujenga mazingira ya kusukuma album ya Arrow Bwoy, na kujitetea kuwa amekuwa akitoa ngoma kali ambazo zimependwa na mashabiki wengi.

Aliwataka mashabiki wake kukubali kwamba muziki ni sanaa na kwamba msanii lazima afanye mambo yasiyo ya kawaida ili kuzidi kutamba.

Alitoa ahadi kwa mashabiki wake kwamba atazidi kutoa muziki mzuri wa kuwaburudisha na kusisitiza kwamba muziki mzuri hauhitaji kiki ili kukubalika.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved