Mwanaume mmoja kutoka kaunti ya Kakamega amewafurahisha watumiaji wa mtandao wa Twitter wakati alipoweka wazi kwamba baada ya kushinda mchezo wa kamari katika jukwaa la SportPesa, aliamua kutumia kiasi hicho kulipa mahari ya mkewe na masalio kujenga bafu na choo.
Zablon Shitanda, mwenyeji wa Malaba aliwekeza katika mchezo huo wa spoti na kujishindia kiasi cha elfu 238,778 pesa za Kenya mnamo mwezi wa tisa mwaka jana na kusema kwamba hajutumii kwa jinsi alivyoratibu matumizi ya hela hizo.
“Mimi ni shabiki wa SportPesa niliweza kuwekeza na juzi mwezi wa tisa nilishinda shilingi elfu 238 kutoka jukwaa la SportPesa. Kwa hiyo pesa niliweza kupeana mahari ya ng’ombe, hata sasa hivi kwa boma yangu nimejenga bafu na choo ya SportPesa,” anasikika akisema katika video ambayo jukwaa hilo kubwa la ubashiri nchini lilipakia kwenye ukurasa wao wa Twitter.
Katika video hiyo, watu wametoa maoni yao tofauti tofauti. Kuna wale wanaompongeza kwa hatua hiyo ya kutumia pesa kwa mambo ambayo yanaweza elezeka kwa miaka na mikaka ijayo huku baadhi wakitofautiana na yeye kwa kusema kwamba angenunua kwanza simu nzuri.
Ama kwa kweli watu hawafanani katika fikira na mawazo!
