logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ibraah na Anjellah ni wajukuu wangu - Diamond Platnumz

Diamond Platnumz amesema kwamba IBraah na Anjellah wa Kondegang ni wajukuu wake.

image
na Davis Ojiambo

Burudani21 April 2022 - 05:50

Muhtasari


  • • Diamond Platnumz amesema kwamba Ibraah na Anjella ni kama wajukuu wake.
  • • Amempongeza Harmonize kwa kulea vipaji vya chipukizi mbalimbali.
Diamond Platnumz

Mwanamuziki matata kutoka Tanzania, Diamond Platnumz amesema kwamba wasanii, Ibraah na Anjellah kutoka Kondegang ni kama wajukuu wake.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha BBC huko London, Platnumz alisema kwamba kwa kuwa yeye ndiye aliyemtambulisha Harmonize kwa gemu la burudani na kumpa umaarufu basi moja kwa moja Ibraah na Anjellah wanakuwa wajukuu wake kimuziki.

Kauli hiyo ya Simba ilijiri wakati yupo Uingereza kwa ajili ya kuuza EP yake ya FOA, katika soko la ughaibuni.

Alimpongeza Harmonize kwa juhudi zake za kuwashika mkono chipukizi wengine kwenye muziki.

Wiki chache zilizopita katika hafla ya tuzo za muziki huko Tanzania, Harmonize alikiri kwamba huenda watu wasingemfahamu iwapo Diamond Platnumz hangejitolea kumsaidia, kauli hiyo ikionyesha umuhimu wa Simba katika maisha ya Kondeboy.

Ibraah na Anjellah katika siku za hivi karibuni wameonekana kutia juhudi nyingi sana kwenye kazi zao huku kibao cha majuzi kutoka kwa Ibraah [Rara] kiliweka rekodi ya views milioni moja chini ya saa moja.

Je, wewe kama shabiki na mshikadau wa burudani unakubaliana na kauli ya Diamond Platnumz?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved