Binti ya Mwenyekiti wa chama cha United Democratic Alliance Johnson Muthama Janet Nthoki amefariki.
Habari za kifo chake zilitangazwa kwa mara ya kwanza na Naibu Rais William Ruto mnamo Jumanne.
Alimtaja Janet kuwa ni mtu ambaye atakumbukwa kwa bidii, uaminifu na kutegemewa.
"Upendo na maombi yetu kwa Mwenyekiti wa UDA Johnson Muthama kwa kumpoteza bintiye mpendwa Janet Nthoki Nduya. Alikuwa mwanamke mwenye bidii, anayewajibika na mwaminifu ambaye atakumbukwa kwa fadhili na kutegemewa kwake."
Mkuu wa pili amewapa rambirambi familia ya aliyekuwa seneta wa Machakos.
"Familia, ndugu, jamaa na marafiki wapate nguvu ya kupita katika maumivu haya. Pumzika kwa Amani Janet."