logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kifo! Mwanawe mbunge maalum David Sankok ajiua kwa kujipiga risasi

Wimbi la simanzi limegubika boma la mbunge maalum David Sankok baada ya mwanawe kujipiga risasi na kujiua nyumbani kwao katika kaunti ya Narok siku ya Jumatatu. Inasemekana marehemu alitumia bunduki ya babake kujitoa uhai. Polisi, na familia walisema Memusi Sankok alikuwa mwanafunzi wa kidato cha 4 katika Shule ya Upili ya Kericho.

image
na Radio Jambo

Habari02 May 2022 - 15:57
Mbunge maalum David Sankok

Wimbi la simanzi limegubika boma la mbunge maalum David Sankok baada ya mwanawe kujipiga risasi na kujiua nyumbani kwao katika kaunti ya Narok siku ya Jumatatu.

Inasemekana marehemu alitumia bunduki ya babake kujitoa uhai.

Polisi, na familia walisema Memusi Sankok alikuwa mwanafunzi wa kidato cha 4 katika Shule ya Upili ya Kericho.

Maafisa wa DCI walitembelea eneo la tukio kukusanya ushahidi wa kisayansi ili kuanzisha uchunguzi.

Baadaye mwili huo ulitolewa nyumbani.

"Baba hakuwa nyumbani wakati mvulana huyo alijipiga risasi na haijafahamika jinsi alivyoipata bunduki ambayo ingepaswa kulindwa ipasavyo," afisa mkuu anayefahamu kisa hicho alisema.

"Alikuwa na umri wa miaka 15. Alijipiga risasi na kufa nyumbani kwao. Hatujui nia gani, "afisa mwingine alisema.

Duru za familia zilisema kuwa mtoto huyo wa kiume na babake wamekuwa na tofauti kuhusu utendaji wake katika masomo.

Polisi walisema wanachunguza nia ya tukio hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved