logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa anayedaiwa kumpiga mwenzake kwa kuwa na msimamo tofauti wa kisiasa akamatwa

Mshukiwa anaripotiwa kuwa mfuasi wa mbunge wa sasa wa eneo hilo Fred Ouda.

image
na Radio Jambo

Burudani21 June 2022 - 02:44

Muhtasari


•Jamaa huyo alikamatwa Jumatatu kufuatia kisa hicho kilichotokea hapo awali  katika mtaa wa Nyalenda.

•Polisi wameanzisha msako wa kumtafuta mtu aliyekuwa akirekodi video hiyo.

Polisi katika kaunti ya Kisumu wanamzuilia Jamaa ambaye alinaswa kwenye kanda ya video akimpiga mwenzake kwa kuwa na msimamo tofauti wa kisiasa amekamatwa.

Jamaa huyo alikamatwa Jumatatu kufuatia kisa hicho kilichotokea hapo awali  katika mtaa wa Nyalenda.

Mzozo ulichimbuka baada ya mhasiriwa kuweka wazi kwamba anampendelea Dkt Joshua Oron kwa kiti cha ubunge cha Kisumu ya Kati.

Mshukiwa anaripotiwa kuwa mfuasi wa mbunge wa sasa wa eneo hilo Fred Ouda.

Kamanda wa polisi wa eneo la Nyanza, Karanja Muiruri alisema idara yake imeanzisha msako wa kumtafuta mtu aliyekuwa akirekodi video hiyo.

Muiruri aliongeza kuwa mshukiwa yuko rumande akisubiri kufikishwa mahakamani.

Pia alisema watarekodi taarifa ya mhasiriwa kuhusu kile kilichojiri.

Video hiyo iliyosambaa kwenye mtandao ya kijamiii inaonyesha mhasiriwa akichapwa viboko na kulazimishwa kujitolea kumuunga mkono mbunge Ouda.

Katika taarifa ya mapema, mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati aliwataka Wakenya wote kuepuka vitendo vya ghasia tunapoelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9, mwaka huu.

"Wagombea wote, vyama vya siasa, wafuasi wa wagombea, Serikali na kwa hakika Wakenya wote wana wajibu wa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi na kuepuka ghasia, vitisho na kulipiza kisasi ambavyo vinaweza kujumuisha uendeshaji wa uchaguzi huru, wa haki na wa amani. ," alisema.

Chebukati alionya kuwa huenda vitendo hivyo vikahatarisha usalama wa nchi.

Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) pia imewaonya wanasiasa dhidi ya kuendeleza vurugu, huku ikisema kwamba huu sio wakati wa vurugu kama nchi,inapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Agosti.

Jumatatu tume hiyo ililaani vurugu vilivyotokea Jumapili katika uwanja wa Jacaranda jijini Nairobi ambako naibu rais William Ruto alikuwa ameandaa mkutano.

NCIC ilisema kwamba imeanzisha uchunguzi kuhusiana na vurugu hivyo huku pande mbili za siasa maarufu kiendelea kunyoosheana kidole cha lawama.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved