logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) Mwanaume amshtumu mkewe kwa kumpakulia chakula kidogo, aingia na kujipakulia

Klipu hiyo ilizua mjadala mkali huku baadhi wakiuliza mbona wanawake wanapakua chakula kidogo kwa waume zao licha ya kuwa wao ndio hununua chakula hicho nyumbani.

image
na Radio Jambo

Michezo26 August 2022 - 06:49

Muhtasari


•Mwanaume huyo anaonekana kwenye klipu akiteta vikali dhidi ya chakula kidogo alichopakuliwa na mkewe.

• Kwa ghadhabu anaingia jikoni na kuchukua sheria mkononi kwa kujipakulia mwenyewe.

Video ya mwanaume mmoja akiteta vikali dhidi ya uamuzi wa mkewe kumpakulia chakula kidogo imezua vicheko mitandaoni huku watu wakigawanyika katika makundi kuhusu suala la wake kuwapakulia chakula kidogo waume zao licha ya kufanya kazi ngumu na pengine kuwa wao ndio wanunuzi wa hivyo vyakula nyumbani.

Klipu hiyo iliyopakiwa kwenye mtandao wa Twitter inaonesha mwanaume mmoja mwenye asili ya taifa la Nigeria akiwa na pensi peke yake huku kifua wazi. Mwanaume huyo kwa lugha ya mama anaonekana akiteta vikali huku akichukua sheria mkononi ya kujipakulia mwenyewe kiasi cha chakula ambacho anaona ndicho stahili.

Msosi huo ambao ni mchanganyiko wa wali kwa nyama pamoja na tukio zima la mwanaume kuwa tumbo wazi akiteta huku anajilimbikizia chakula kwenye sinia kubwa imezua mjadala mkali mitandaoni huku watu wakisema wanaume wengine wana pupa na msosi wa nyama huku wengine wakimtetea kwamba kutokana na muonekano wake ni mtu anayejishughulisha na kazi ngumu inayofanya mwili kuhitaji chakula cha kutosha.

“Kuna nini kwa wanaume na nyama? Ona jinsi anavyoropoka kama pumba aliyeharibika. Ina maana kwamba watu wengine pia hawapaswi kula nyama hiyo? Ana bahati hata kupata vipande viwili vya nyama,” mmoja alisema.

“Hili jambo linanishangaza pia nilitaka kumlalamikia mke wangu.. chungu ambacho kina bata mzinga changanya na kuku na konokono, namaanisha konokono wengi lakini nitaishia kuhudumiwa vipande viwili tu. Lakini kila mara nataka kulalamika, nitakumbuka maneno ya mama yangu, nyama haileti afya ya mtu.” Alisema mwingine kwa utani.

Aidha wengine walisema kwamba hio ni igizo lililonakiliwa vizuri na mwanaume huyo katika tukio zima jinsi anavyoteta anaonekana kabisa anajaribu kuigiza.

“Lakini imeandikwa sasa. Ikiwa ni kamera ya ukweli utajua. Kuna dalili za wazi za kuigiza hapa. Jinsi anavyozungumza inaonyesha inaigizwa. Ni watu wachache tu wanaoweza kuigiza na hutajua kuwa iliandikwa na kuigizwa,” mwingine alisaili uhalisia wa klipu hiyo.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved