logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) Nadia asherehekea mwanawe kufikisha miezi 6, amchezea densi

“Mr Handsome ana miezi 6. Nakupenda sana mtoto wangu Kai - Nadia Mukami.

image
na Radio Jambo

Burudani26 September 2022 - 11:48

Muhtasari


• Wewe ni furaha yangu na najivunia kuwa mama yako,” Nadia Mukami aliandika kweney video hiyo. - Nadia Mukami.

Nadia Mukami na Arrow Bwoy kuachia wimbo kwa ajili ya mwanao

Malkia wa miziki ya kizazi kipya nchini Nadia Mukami amepakia video nzuri kwenye ukurasa wake wa Instagram akimchezea densi mwanawe na kumsherehekea kufikisha miezi sita tangu kuzaliwa.

Katika video hiyo, Mukami alionekana akicheza kwa mbwe mbwe na Kai amefungwa kifuani mwake. Mukami alikuwa anacheza kwa wimbo wake mpya ambao aliutoa wiki jana akimshirikisha mpenzi wake Arrow Bwoy, wimbo kwa jina Kai Wangu.

Mukami alimsifia mwanawe kuwa ni mtanashati sana tangu siku ya kwanza na kufichua ilikuwa furaha kubwa kuishi naye katika kila sekundw iendayo kwa Mola katika miezi sita iliyopita.

Mama huyo alisema kama familia, yeye na mumewe Arrow Bwoy waliamua kumrushia bonge la tafrija mtoto wao kushereheka miezi sita na bata la tafrija hiyo litaliwa nje ya Nairobi ili kumbadilishia mazingira na kumjengea kumbu kumbu za utotoni nzuri ajabu.

“Mr Handsome ana miezi 6 😌♥️ Tuliamua kwenda kusherehekea nje ya Nairobi♥️🌺 Nakupenda sana mtoto wangu Kai, wewe ni furaha yangu na najivunia kuwa mama yako,” Nadia Mukami aliandika kweney video hiyo.

Wapenzi hao wenye umaarufu sana mitandaoni, kulingana na kipengele kwenye wimbo huo wa Kai walianza mahusiano yao fiche takribani miaka miwili iliyopita.

Hadi miezi michache iliyopita walipokuwa wanazindua wakfu wao wa Lola na Safari walifunguka kwamba waliwahi poteza ujauzito wao wa kwanza, mimba ambayo walikuwa wanategemea mtoto kuchukua jina moja kati ya hayo ya Wakfu wao kulingana na jinsia – Lola akiwa wa kike na Safari wa kiume.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved