logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ebola Uganda: Museveni aondoa uwezekano wa kuweka karantini

Museveni alisema serikali yake ina uwezo wa kudhibiti janga hilo.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri29 September 2022 - 05:35

Muhtasari


•Ebola huenezwa kwa njia ya kugusana na mtu aliyeambukizwa au sehemu zilizoambukizwa na kinyesi cha binadamu.

•Wahudumu sita wa afya waliomtibu mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye baadaye alitambuliwa kuwa kisa cha kwanza, wamepimwa na kukutwa na Ebola.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hakuna haja ya kuweka vikwazo katika maeneo hatarishi ya Ebola katika eneo la kati kwa sababu ugonjwa huo unaosababishwa na virusi hautokei hewani.

Ebola huenezwa kwa njia ya kugusana na mtu aliyeambukizwa au sehemu zilizoambukizwa na kinyesi cha binadamu.

Chama cha wafanyikazi wa matibabu nchini humu awali kilitoa wito kwa eneo lililoathiriwa kuwekwa karantini ili kukomesha kuenea zaidi kwa homa ya kuvuja damu.

Bw Museveni alisema serikali yake ina uwezo wa kudhibiti janga hilo kutokana na uzoefu wa awali wa milipuko kama hiyo.

Hii ni mara ya nne kwa Ebola kuzuka nchini Uganda. Alisema wataalam wa afya ambao hapo awali walishughulikia milipuko ya Ebola wametumwa katika eneo lililoathiriwa.

Kwa sasa inachukua saa 24 kwa sampuli kufanyiwa uchunguzi na matokeo ya maabara kutolewa.

Rais alisema serikali itafungua maabara katika makao makuu ya wilaya ya Mubende, kitovu cha mlipuko huo, ili kuharakisha usindikaji wa sampuli.

Wahudumu sita wa afya waliomtibu mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye baadaye alitambuliwa kuwa kisa cha kwanza, wamepimwa na kukutwa na Ebola.

Jumla ya watu 24 wamethibitishwa kuambukizwa na virusi hivyo nchini humo, watano kati yao wamefariki tangu kuzuka kwa ugonjwa huo wiki iliyopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved