logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zingatia mambo haya matano kama hutaki kunenepa msimu wa Krismasi

Epuka vinywaji baridi na pombe kupita kiasi kila siku.

image
na Radio Jambo

Burudani21 December 2022 - 03:43

Muhtasari


•Nyakati kama hizi baadhi ya watu wanakabiliwa na kibarua kigumu kufuata utaratibu wao wa kawaida hasa katika masuala ya lishe.

•Ili usiongeze uzani kupita kiasi msimu wa siku kuu za Krismasi na mwaka mpya zingatia vidokezi hivi vitano.

Msimu wa siku kuu za Krismasi huwaleta Pamoja ndugu jamaa na marafiki, katika mikusanyiko kama hiyo vyakula na vinywaji vya kila aina huandaliwa ili kunogesha siku kuu.

Nyakati kama hizi baadhi ya watu wanakabiliwa na kibarua kigumu kufuata utaratibu wao wa kawaida hasa katika masuala ya lishe. Kutokana na hilo mtindo wa maisha hubadilika na hapo ndipo uzito wa mwili pia uweza kubadilika.

Ni nyakati hizi pia ambapo utasikia kusikia jamaa na marafiki wakiwa na wana mazoea ya kusema "nitaanza kesho", msemo ambao unaweza kuendeleza tabia zisizofaa.

Lakini je unawezaje kufurahia msimu wa Krismasi bila kuathiri mpango wako wa afya?

Kwanza kabisa ukiwa na nia ya dhati ya kudhibiti uzani wako lazima ujiwekee mipaka katika ulaji wako ili kuimarisha malengo yako, anasema mtaalamuwa lishe bora Irine Nduta kutika Kenya.

''Ni vyema kuachana na mienendo ambayo haiendani haziendani na malengo yako.''

Ili usiongeze uzani kupita kiasi msimu wa siku kuu za Krismasi na mwaka mpya zingatia vidokezi hivi vitano.

1. Chagua vyakula usile kila kitu

Ni muhimu pia kufahamu kuwa unaweza kuteleza mara moja au mbili katika safari hii ya kudhibiti uzani anasema mtaalamu wa lishe bora Bi Nduta.

Mara nyingi watu huachana na malengo yao baada ya hili kutokea.

Lakini, ni bora kuendelea kuzingatia lishe bora kuliko kurudi nyuma.

2. Kula kwa kipimo

Punguza vyenye wanga katika sahani yako ikiwezekana kwa karibu theluthi tatu, kile kinachoitwa sheria ya udhibiti wa chakula ili kuboresha afya.

Unaweza kifikia lengo hili kwa kujizoesha kula chakula kidogo kwa saa chache za siku au kufunga na kula katika masaa manane kwa siku au kufunga kula chakula siku mbili kwa wiki.

Hii ni mambo yanayoaminiwa kupunguza hatari ya kupata magonjwa yanayohusiano na umri.

3. Jifuatilia mwenyewe

Ingawa kuzingatia malengo ya kudhibiti uzani kunaweza kuwa kibarua kigumu wataalamu wa masuala ya afya wanasema.

Ni vyema kuhakikisha kuwa unapunguza ulaji wa vyakula vya vilivyokaangwa kwa kutumia mafuta mengi wakati wa likizo.

4. Fanya mazoezi

Maisha ya kutofanya mazoezi ya mwili husababisha 10% ya vifo vya mapema vinavyotokana na magonjwa kama vile ugonjwa wa moyo, kisukari aina ya mbili, na aina mbali mbali za saratani. 

Hakikisha unatembea au kuogelea hali ya hewa ikiauhusu, na epuka kutumia kipindi cha sherhe kukaa mahali pamoja.

5. Usinywe pombe

Epuka vinywaji baridi na pombe kupita kiasi kila siku.

Unapokunywa pombe hakikisha unakunywa maji pia kati ya kila kinywaji cha pombe.   

Ukizingatia malengo yako kwa bidii, unaweza kupata kwamba umefanikiwa kudhibiti uzani wako hata wakati wa msimu huu wa sherehe.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved