logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nialike kwa shoo zenu, nahitaji kujivinjari - Rais mstaafu Jakaya Kikwete awaomba wasanii

Kikwete alitoa wito huu wakati wa kuhudhuria shoo ya msanii Marioo

image
na Radio Jambo

Burudani02 February 2023 - 07:01

Muhtasari


• "Napenda muziki mzuri kwa hivyo sijali mialiko zaidi kwa sababu nitahudhuria kwa makusudi.” - Kikwete alisema.

katika picha ya maktaba

Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa wasanii haswa wa Bongo Fleva kutoogopa kumpa mialiko ya kuhudhuria shoo zao kwani naye ni kama binadamu mwingine yeyote tu anayehitaji kujivinjari na kujifurahisha.

Kikwete ambaye alirithiwa na hayati Magufuli si mara ya kwanza anaonekana akijitokeza hadharani kuzipigia shoo za wasanii debe.

Mwaka jana wakati wa kuzinduliwa kwa albamu ya Dedication yake msanii Ommy Dimpoz, rais Kikwete alikuwa mgeni mashuhuri na alijitokeza kuipaisha hafla hiyo ya uzinduzi wa albamu.

Wikendi iliyopita, wakati wa shoo ya Marioo, Kikwete pia alitokea na kutoa ombi kwa wasanii kutomuogopa bali kuendelea kumpa mialiko ili kuhudhuria shoo zao.

“Nataka kuwashukuru nyinyi kwa mitoko mnazoniongezea; Ninawapenda. Nasema hivi kwa sababu kwa baadhi yetu maisha yetu yamekuwa magumu kidogo. Unaishi kwenye nyumba ambayo imezungushiwa ukuta mkubwa wa pembeni kisha kuna nyingine katikati na nyingine inayozunguka nyumba unayoishi,” Kikwete aliiambia hadhara hiyo.

"Kwa hivyo, kila ninapopata mialiko kama hii, ninafurahi sana kwa sababu ni fursa adimu kwangu kwenda nje usiku, kuwa mimi mwenyewe, kupumzika na kuwa na wakati mzuri. Ninamaanisha kuwa ni usiku mzuri wa burudani na napenda muziki mzuri kwa hivyo sijali mialiko zaidi kwa sababu nitahudhuria kwa makusudi.”

Kikwete mwenye umri wa miaka 72 mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu nchini Kenya, aliongoza timu ya waangalizi wa kimataifa ambao walitumwa na AU kuangalia jinsi shughuli za uchaguzi nchini zilikuwa zinzfanyika kisha kuwasilisha ripoti.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved