logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Andrew Kibe bila kunitukana hana kazi, na vile yeye ni maskini - Diana Marua

โ€œNimegundua kuwa Bila kumtaja Diana B! huyu jamaa atakuwa hana Kazi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ ni sawa!โ€

image
na Davis Ojiambo

Burudani05 March 2023 - 10:13

Muhtasari


  • โ€ข โ€œAndrew Kibe hakim bona unapenda kunitukana na vile wewe ni maskini?โ€
Marua amjibu Kibe

Diana Marua kwa mara ya kwanza amemjibu mwanablogu Andrew Kibe vikali kufuatia madai ambayo mwanablogu huyo mkaazi wa Marekani amekuwa akitupa kwa familia ya Maruac na mpenzi wake Bahati kwa muda mrefu sasa.

Kibe amekuwa akieneza uvumi kwamba Marua anamtawala Bahati na anamchukulia kama mtoto wake, kitu ambacho amekuwa akimtuhumu Bahati kwa kukubali kutawaliwa na mwanamke.

Kwa muda wote huu, familia ya Bahati na Marua haijawahi kumjibu Kibe lakii safari hii ni kama Kibe alikanyaga pabaya, mpaka kumghasi Marua ambaye amevunja kimya chake.

Kulingana na Marua, amegundua kwamba Kibe hawezi pata kitu cha kuzungumzia kwenye blogu yake ya YouTube pasi na kujadili kile ambacho kinaendelea katika familia yake.

“Nimegundua kuwa Bila kumtaja Diana B! huyu jamaa atakuwa hana Kazi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ ni sawa!” Diana Marua alizua.

Alizidi kwa kumsimanga vikali Kibe akisema kwamba yeye ni maskini sana kumliko, lakini haoni hilo bali kazi yake kumzungumzia kwa mabaya na chuki.

“Andrew Kibe hakim bona unapenda kunitukana na vile wewe ni maskini?” Diana Marua aliuliza kwa upole lakini kwa sauti iliyojawa kejeli na kebehi.

Kibe amekuwa akimzungumzia Marua kwa njia hasi, kumuita mzee kwa mume wake Bahati.

Lakini si yeye peke yake ambaye Kibe amekuwa akipiga mabomu ya moto. Mwanablogu huyo mwenye utata mwingi amekuwa akiwaingilia watu mashuhuri Kenya kwa njia ya aina yake, huku akionekana kufurahia kila mara watu hao wanapopatikana kwenye kashfa au skendo.

Baadhi ya wanamitandao walisema wangependa kumuona Kibe akijibu hilo, huku wakisema mwanablogu huyo atajibu kwa ukali kwani tayari ameshapata kitu cha kuzungumzia kwenye blogu yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved