logo

NOW ON AIR

Listen in Live

East Africa Specter Limited inayomilikiwa na Raila yashambuliwa na watu wasiojulikana

Uchunguzi zaidi kuhusu suala hilo unaendelea.

image
na Radio Jambo

Burudani27 March 2023 - 12:24

Muhtasari


  • Katika video inayosambaa mitandaoni madirisha kadhaa yalivunjwa na mawe yaliyotapakaa lango la kiwanda hicho.

East Africa Specter Limited, kiwanda cha gesi kinachoaminika kumilikiwa na kiongozi wa Azimio Raila Odinga, kilishambuliwa Jumatatu baada ya watu wasiojulikana kupiga mawe sehemu ya mali hiyo.

Katika video inayosambaa mitandaoni madirisha kadhaa yalivunjwa na mawe yaliyotapakaa lango la kiwanda hicho.

Kanda nyingine ya CCTV inaonyesha idadi ya watu takriban 20 wakirusha mawe nje ya lango.

Meneja wa ulinzi na usalama katika kampuni hiyo Humphrey Waswa alisema kuwa watu hao walifika eneo hilo wakiwa na pikipiki na kuanza kurusha mawe kwa takriban dakika 30 kabla ya askari polisi kufika na kuwatawanya watu hao.

"Walikuwa wakisaidiwa na magari manne yasiyokuwa na alama (land cruiser) na tunashuku lengo lao lilikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wetu kwa sababu ofisi yake imeharibiwa zaidi," alisema.

Uchunguzi zaidi kuhusu suala hilo unaendelea.

 

 

 

 

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved