Mwimbaji tajiri wa Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P amedokeza kurudiana na mwanamitindo kutoka Ivory Coast Eudoxie Yao.
Katika picha alizochapisha kwenye akaunti yake wawili hao wakipata chakula pamoja na ujumbe kuwa mapenzi hayaishi.
“True Love never ends” aliandika Grand P kwenye picha aliyoweka kwenye Facebook.
Mashabiki wa mwanamziki huyo mwenye umbile la mbilikimo waliwasherehekea kurudiana kwao.
Aprili mwaka huu Grand P alitangaza kuingia katika uhusiano na mwanadada mwingine mwenye asili ya Kiasia, Yubai Zhang.
Grand P alitangaza mahusiano yao kupitia akaunti yake ya Facebook akithibitisha mapenzi yake na mrembo huyo wa Kiasia na kuweka wazi kuwa hakuna nafasi ya watu wenye wivu maishani mwao.
"Yubai Zhang wangu, hakuna nafasi kwa watu wenye wivu," alisema chini ya picha zake na Zhang alizochapisha Facebook.
Balozi huyo wa Guinea nchini Mali alikatisha mahusiano yake na mwanamitindo Yao mwaka wa 2021 baada ya kuwa kwenye mahusiano na mwanamitindo huyo kwa takriban miaka mitatu.
Wawili hao walitangaza kukuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka wa 2020 baada ya kuchapisha picha wakiwa pamoja.
Mahusiano hayo yaliibua gumzo mitandaoni kwa ajili ya uzani wao, mashabiki walishangaa ni vipi Grand P mweye mwili mdogo anaweza kuwa kwenye mahusiano na mwanamke huyo aliyeonekana kumzidi kwa uzani kwa kiasi kikubwa.
Lakini licha ya wafuasi wao wengi kutokubaliani na chaguo la Grand P la kuchumbiana na Yao, wawili hao walisisitiza kuwa wana furaha na wataendelea kuwa kwenye mahusiano.
"Tuna Furaha tukiwa pamoja, na hicho ndicho kitu cha maana. Asante kwa kila mmoja wenu kwa msaada wenu, ya kimwili haihesabiki katika mahusiano” aliandika Yao katika akaunti yake ya Instagram.