logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee aweka wazi kufanya kolabo na Babake, Jose Kokeyo

Akothee alionyesha kufurahishwa sana na sauti ya baba yake hivyo basi alionekana akisifia sauti yake.

image
na

Burudani10 July 2023 - 06:24

Muhtasari


• Hili linajiri baada ya Akothee kupakia video katika ukurasa wake wa Instagram akielezea kuwa wanatayarisha remix na baba yake.

Akothee aweka wazi kufanya kolabo na babake, Jose Kokeyo

Siku ya Jumapili, mwanamuziki na mfanyabiashara mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee aliweka wazi katika kufanya remix na baba yake, Jose Kokeyo.

Hili linajiri baada ya Akothee kupakia video katika ukurasa wake wa Instagram akielezea kuwa wanatayarisha remix na baba yake.

Mwimbaji huyo amekuwa akifurahia wakati na baba yake katika nyumba yake ya kifahari iliyo eneo la Rongo, Kaunti ya Migori katika siku chache zilizopita.

Mwanamuziki huyo alionyesha kufurahishwa sana na sauti ya baba yake hivyo basi alionekana akisifia sauti yake.

'Wao ❗wao❗ wao❗ wao , tulikaa na baba yangu siku nzima studio tukitengeneza upya Nyimbo zake Ft Akothee 🙏Baba yangu ana sauti za wazimu.

Nani anasubiri hii Mash up. Shukrani kwa Wuod Fibi kwa kuwezesha hili Barikiwa saba Chuor Nyanyakach 🙏Jiandikishe kwa kituo changu cha YouTubeLink kwenye Bio yangu.Akothee Ft JOSI KOKEYO wa Ranen Jasband 👏👏👏👏👏💪," aliandika Akothee kwa mbwembwe.

Wanamitandao wengi walionekana wakimsifia na kumpongeza Akothee kwa kitendo hicho.

"Hongera kwa kumpenda baba yako Mungu atakupa maisha marefu na heri," alimhongera christinamsoka436.

"Gwiji Jose Kokeyo🔥tulikuwa na wakati mzuri wa kurekodi miaka yake ya nyuma," sapatdiary aliandika.

"Mzee anaonekana mnyenyekevu Mungu ambariki," aliandika blessd_gal_254.

"Madam boss mwenyewe na baba yake ❤️😍," kingchachadollar alinena.

"Hizo remix zitakua🔥," sapatdiary aliandika.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 amekuwa akirekodi na kushiriki baadhi ya nyakati zake nzuri na mzazi huyo wake na anaonekana kufurahia sana kila dakika anayoshiriki na mwanamume huyo aliyemlea.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved