logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vera Sidika na mwigizaji Kate Actress washinda Tuzo Nchini Nigeria

Vera Sidika  alishinda tuzo ya Sosholaiti  mashuhuri Afrika 2023

image
na

Burudani30 November 2023 - 05:45

Muhtasari


•Wawili hawa walionyesha furaha yao kwenye mitandao yao ya instagram huku wakishukuru wote ambao waliwapigia kura kufanikisha ushindi huo.

Vera Sidika na Kate Actress.

Sosholaiti  Vera Sidika  na muigizaji  Kate Actress wameshabikia ushindi baada ya kuibuka washindi katika Tuzo tofauti za Wanawake mashuhuri Afrika 2023  tuzo ambazo zilipeanwa Nchini Nigeria.

Wawili hao walionyesha furaha yao kwenye mitandao yao ya instagram huku wakishukuru wote ambao waliwapigia kura kufanikisha ushindi huo.

Vera Sidika alisherehekea kwa kushinda tuzo ya Sosholaiti  mashuhuri Afrika katika taji la tuzo za Africa Women  Awards 2023  nchini Nigeria.

Sidika aliwashida waigizaji wanne wa Nigeria na kutwaa taji hilo,Sosholaiti huyo wa mwaka 2023 alitoa shukrani zake kwa kuwashukuru mashabiki wake kwa kumpigia kura.

"Asanteni sana kwa kila mtu aliyenipigia kura kunyakuwa tuzo hiyo,"aliandika kwenye  instagram.

Kwenye tuzo ya pili Mwigizaji Catherine Kamau almaarufu  Kate Actress alishinda taji la Mwigizaji bora wa kike  mwaka 2023  katika Tuzo za Wanawake wa  Afrika.   Kate  alishindana na waigizaji tisa kutoka Nigeria, kuku akiibuka kama Mkenya pekee aliyeteuliwa katika kitengo hicho.

Akielezea furaha yake baada ya kutangazwa mshindi, Kate alitoa shukrani zake kwa mashabiki wake.

 "Mmeamua ni wow! wow! wow! design ya ambulance mwaka mzima, Thank you Fam," Kate aliandika kwenye mtandao wake.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved