logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bien kutumbuiza mashabiki wake ulaya, katika ziara yake ya kwanza nje ya Sauti Sol

Bien kuanza ziara yake ya Ulaya pekee yake mwezi wa machi 7.

image
na Radio Jambo

Burudani22 February 2024 - 09:29

Muhtasari


  • Bien alionyesha furaha yake kukuwa na ziara ya Ulaya pekee yake kwa mara ya kwanza kabisa.

Mwanachama mwanzilishi wa bendi ya Sauti sol Bien-Aime  Baraza ametangaza ziara ya Ulaya pekee yake kuanzia mwezi wa Machi mwaka huu.

Ziara hiyo imepewa jina la  "Alusa Why Are You Topless"  ambayo ni sawa na albamu yake ya hivi punde. Atakuwa anaangazia wanamuziki wawili wa Afrika Mashariki; Xenia Manasseh wa Kenya na Joshua Baraka wa Uganda.

Wakati akitoa tangazo hili kwenye Instagram, Bien alionyesha furaha yake kukuwa na ziara ya Ulaya pekee yake kwa mara ya kwanza kabisa.

"Afrika Mashariki inavuma kwa vipaji vinavyoongezeka vya nyimbo za R&B na moja ya malengo yangu imekuwa daima kubeba Afrika Mashariki pamoja nami kila mahali ninapokwenda", Aliandika.

"Nina Furaha kuleta @xeniamanasseh na @itsjoshuabaraka nami kwa ziara yangu ya kwanza ya Uropa inayoanza mwezi ujao".

Alifichua kwamba Kenya Airways itakuwa wadhamini rasmi wa tamasha hilo linalotarajiwa bara uropa. 

" Mapenzi tele kwa @kenyaairways, wadhamini rasmi wa tamasha langu. Nyinyi nyote mmewezesha hii kitu yote. Keki ni kubwa ya kutosha kwa kila mtu basi tule!!" Bien alimalizia.

Baadhi ya miji ya Ulaya ambayo atatembelea ni ; Paris, Rotterdam,Brussel, Cologne, Berlin, London, Copenhagen and Uppsala.

London tayari ticketi zote zimeuzwa. Copenhagen mji wa Denmark na Uppsala mji wa Sweden asilimia tickiti 90 zimeuzwa.

Joshua Baraka na Xeniah Manasseh walielezea mashabiki wao katika mtandao wa kijamii  vile wamefurahia kushiriki kwenye ziara ya Bien ya pekee Ulaya.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved