logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msanii Sabato amuunga mkono Chingiboy kuendelea kushikilia akaunti za Simple Boy hadi alipwe

Sabato alidai kuwepo na kushuhudia jinsi Chingiboy alivyokuwa akihangaikia akaunti hizo.

image
na Radio Jambo

Burudani08 April 2024 - 13:19

Muhtasari


• Sabato alidai kuwepo na kushuhudia jinsi Chingiboy alivyokuwa akihangaikia akaunti hizo.

• Wiki jana, Chingiboy alifichua kwamba anataka kufidiwa shilingi laki moja na nusu pesa za Kenya kwani ndicho kiasi alichotumia kuzikomboa akaunti hizo.

Sabato Sabatoo

Msanii Sabato Sabato amekuwa mtu kutoka tasnia ya muziki wa Kenya wa hivi karibuni kuweka kwenye mizani suala linalozidi kugonga vichwa vya habari kuhusu sakata la msanii Stevo Simple Boy na aliyekuwa meneja wake, Chingiboy Mstado.

Katika video moja, Sabato alionekana akipigia debe hatua ya meneja huyo kukwama na akaunti za mitandao ya kijamii za Stevo Simple Boy baada ya uhusiano wako wa kikazi kusambaratika siku chache zilizopita.

 Sabato alisema kwamba Chingiboy alifanya jambo la muhimu kushikilia akaunti hizo ikiwemo YouTube na Instagram kwani alitumia pesa nyingi kuzikomboa kutoka kwa uongozi wa awali baada pia ya kushindwa kuendelea kufanya kazi na msanii huyo.

Sabato alisema kwamba Chingiboy aendelee kushikilia akaunti hizo hadi pale familia ya msanii huyo itakapomlipa kiasi cha pesa alizotumia kukomboa akaunti hizo, akidai wanafamilia wamekuwa wakimhadaa Stevo.

“Sasa hivi mimi nataka kumuambia Chingiboy, usipatiane hizo akaunti, usipatiane kitu kama hujapatiwa pesa zako. Rudishieni Chingiboy pesa zake kwa sababu nasikia watu wameanza kumpiga mikwara. Mimi nilikuwa naona vile Chingiboy alikuwa anahanaika sana,” Sabato alimuunga mkono Chingiboy.

Aidha, katika mazungumzo na Moses Sagwe wa Radio Jambo, Chingiboy alithibitisha madai hayo ya Sabato kwamba amekuwa akitishiwa tangu wiki jana alipoweka wazi kushikilia akaunti za mtandaoni za Stevo.

Chingiboy alisema kwamba amekuwa akitumiwa watu kumpiga mikwara kuhusu suala hilo la kushikilia akaunti za Instagram na YouTube za Stevo Simple Boy lakini akasema hayuko tayari kuzama kwa mikwara yao.

Meneja huyo ambaye pia ni msanii alisisitiza kwamba ataachilia akaunti za Instagram na YouTube za Stevo Simple Boy hadi pale atakapofidiwa Ksh 150K alizodai kutumia katika kuzikomboa kutoka kwa uongozi wa awali wa MIB uliokuwa unamsimamia Stevo.

“150K, nilinunua hizo akaunti na hicho kiasi cha pesa. Mpaka sasa hakuna mtu kutoka kwa familia ya Stevo amenifuata kuhusu suala hilo lakini wanatuma watu kunipa vitisho,” alisema Chingiboy.

Wiki jana katika mahojiano na blogu moja ya humu nchini, meneja huyo ambaye pia ni msanii alisema alitumia pesa nyingi kwa msanii huyo lakini baada ya kauchana, hataka kurudishiwa pesa alizotumia kwake bali anachokitaka ni kurudishiwa pesa alizotumia kukomboa akaunti zake baada ya kukosana na uongozi wa MIB.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved