logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(Video) Mwinjilisti akimbia kuokoa maisha maji ya bahari yakimfuata wakati wa kurekodi wimbo

Inajiri siku chache baada ya Junior Pope kufa maji akishoot video majini.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 April 2024 - 10:37

Muhtasari


• Katika mandharinyuma ya video hiyo, sauti ya kiume ilisikika ikimwita mwanamke huyo baharini lakini hakugeuka hadi alipotoka ufukweni.

Mwanamke wa Nigeria, ambaye huimba nyimbo za injili, amezua mijadala mtandaoni kuhusu alichiamua kukifanya baada ya tukio lisilotarajiwa kutokea wakati wa kupiga video ya muziki baharini.

Katika video iliyosambaa mtandaoni, mwanamke huyo ambaye hakufahamika jina lake, akiwa amevalia gauni jeupe na kichwa cha rangi ya bluu kichwani, alionekana akionyesha umahiri wake wa kuimba huku akicheza kwa furaha akiwa amesimama kwenye ufuo wa bahari.

Alipokuwa akiimba karibu na ufuo, alikatishwa na msomo wa ghafla wa maji, na kuzua hofu kwa mwimbaji wa nyimbo za injili aliyeingia.

Wakati bahari ilipokuwa inasonga mbele, alikimbia mara moja kuokoa maisha ya thamani alipokuwa akitoka baharini, na kuibua hisia miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Katika mandharinyuma ya video hiyo, sauti ya kiume ilisikika ikimwita mwanamke huyo baharini lakini hakugeuka hadi alipotoka ufukweni.

Video hiyo ilipata mvuto haraka huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakichangia mawazo yao huku wengi wakisimulia jinsi mwigizaji wa Nollywood, Junior Pope, alivyozama na kufa katika ajali ya boti.

 

Tazama video hapa chini:

Kisa hiki cha kujaribu kujiokoa kutoka kwa wimbi la maji ya bahari kinajiri siku chache baada ya tasnia ya filamu Nigeria kupiga marufuku matukio ya ku’shoot video kwenye maji baada ya muigizaji Junior Pope kufa maji wakati wa kuandaa filamu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved