logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maoni mseto Bahati akimtaja babymama wake Yvette Obura kama ‘My Sisiter’ wakati akimuomba radhi

So Mueni is your niece,with due respect to your wife, atleast refer to Yvette as mummy so that Mueni will appreciate it in future."

image
na MOSES SAGWE

Burudani25 October 2024 - 10:39

Muhtasari


  • "So Mueni is your niece,with due respect to your wife, atleast refer to Yvette as mummy so that Mueni will appreciate it in future."

Msanii Bahati Kioko Kelvin amevutia maoni kinzani katika mtandao wa Instageam baada ya kuchapisha msururu wa jumbe za msamaha kuhusu watu ambao anahisi huenda aliwakwaza siku za nyuma.

Bahati alichapisha jumbe hizo akiomba radhi kwa baadhi ya watu ambao alihisi aliwakosea kwa kuvuta majina na sura zao kwenye vimbwanga vyake na mkewe kwenye mitandao ya kijamii.

Mmoja kati ya watu ambao Bahati aliomba radhi ni mzazi mwenzake, Yvette Obura – ambaye wana mtoto mmoja wa kike pamoja, Mueni Bahati.

Hata hivyo, kuomba msamaha halikuwa suala kubwa; kilichozua minong’ono mingi katika chapisho hilo ni jinsi Bahati alivyomtaja Obura.

Msanii huyo alimtaja babymama wake kama’ dadangu’ jambo lililofanya wengi kuzua maneno na kuhoji kwa nini asingemtaja tu kwa jina lake au hata kumtaja kama mzazi mwenzangu kwa kutambua mtoto ambaye amewaunganisha.

“Mnamo Juni 2024 nilichapisha picha ya Yvette Obura kwenye akaunti zangu za mitandao ya kijamii."

Nachukua nafasi hii kumpa pole Dada yangu kwa madhara yoyote yaliyojitokeza. Sikuwahi kuwa na nia mbaya. Ninatazamia kukuza malezi bora ya uzazi katika siku zijazo,” Bahati aliandika.

Ujumbe huu ulionwekana kuwakasirika watumizi wa mtandao huo, wengi wakionekana kumsuta kwa kumtaja babymama wake kama ‘dadangu’ – wakisema huo si msamaha halali bali ni kuongezea dharau zaidi kwenye jina la Obura.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

@jennyet: Yaani hii ni karaha kumwita mama wa mtoto wako dada. Una watoto na dada yako?

@c.karry11: Babymama anakuwa dada Tena! Wanaume mna mambo kweli.

@Umtoni.hadassah: Eeeeeee kumwita dada yako sasa ni kiwango kingine cha kutomheshimu mzazi, mwenzako kweri 

@prin.cessirene1: Eeeh Baha, unathubutu vipi kumtaja Yvette kuwa ni dada yako? So Mueni is your niece,with due respect to your wife,at least refer to Yvette as mummy so that Mueni will appreciate it in future. Si ajabu tu mueni anasomaje hii post na babake anamuita mama dada,hii ni comedy bwana.

Bahati na Yvette walichumbiana kwa muda mfupi na kupata mtoto huyo kabla ya kutengana na akaoana na mrembo Diana Marua.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved