Salasya alisema kwamba kumekuwa na ongezeko la warembo wengi kutumia mtego huo kama kitega uchumi kwa kuwatishia wanaume kuwatumia pesa la sivyo wasivujishe picha na video zao mitandaoni.
Katika chapisho lake kwenye Instagram yake Jumapili, Oktoba 27, 2024, Salasya alionyesha kufadhaika kutokana na hali inayoongezeka ambapo wanawake hurekodi kwa siri matukio ya faraghani na watu binafsi na baadaye kutumia rekodi hizi kama njia ya kujinufaisha kifedha.
Kulingana na Salasya, watu hawa huchukua picha au video za wanaume wakati wa hatari na baadaye kuzituma kama ujumbe wa "tazama mara moja" kwenye WhatsApp.
Wanatumia maudhui kudai pesa na kutishia kuachilia video hizo iwapo matakwa yao hayatatekelezwa.
Mbunge huyo alitaja kuwa mwanamke anaweza kudai Ksh300,000 ili kuzuia kuvujisha kwa picha na video kama hizo.
Mbunge alihoji jibu linalofaa kwa hali kama hizo na jinsi mtu anaweza kushughulikia hali inayokua.
“Hawa wasichana wa kukupiga picha na video ukiwa umelala alafu anakutumia view mara moja baadaye kwa WhatsApp na kukuuliza umupe 300k ama awachilie picha na video tunachukuliaje hii kesi. Halafu anamake sure amechukuwa video strategically kama ume…” Salasya aliuliza.