logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond Platnumz amzawadi Mzee Makosa shilingi milioni 10

Msanii huyo amefanya hivyo baada ya kuguswa na simulizi ya Mzee Makosa ya jinsi aliingia katika dimbwi la umaskini

image
na Brandon Asiema

Burudani30 October 2024 - 08:42

Muhtasari


  • Simulizi ya Mzee Makosa iligusa mioyo ya watu wengi baada ya kusambaa mitandao ya kijamii nchini  Tanzania.
  • Diamond Platnumz alimpa mzee huyo kitita cha shilingi milioni 10 za Tanzania baada ya kutazama simulizi ya Mzee Makosa na kutaka sana kukutana naye angalau kumsalamia mkononi

caption

Msanii wa muziki wa Bongo ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Wasafi Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amemtunuku mzee mmoja kutoka Iringa kitika cha shilingi milioni 10 pesa taslimu za Tanzania.

Diamond amefanya hivo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mzee huyo kwa jina Ramadhani Mrisho aliyevuma kwenye mitandao ya kijamii kutokana na simulizi yake ya maisha ilioonekana kugusa mioyo ya watu wengi.

Mzee Makosa jinsi anavyofahamika na watu wengi, katika mahojiano na kituo kimoja cha mawasiliano cha nchini Tanzania alieleza jinsi aliingia kwenye dimbwi la umaskini kutoka kwenye utajiri aliokuwa nao.

Kwa mujibu wa chombo kimoja cha mawasiliano nchini Tanzania, Diamond Platnumz aliguswa na simulizi ya mzee huyo na alitaka sana kukutana naye  kwa mazungumzo na angalau apate fursa ya kumsalamia mkononi.

Aidha baada ya kupata fursa ya kukutana na Mzee Makosa na hata kuwa na nafasi ya kuzungumza na kumsalamiamkononi jinsi alivyokuwa ametamani, Diamond Platnumz hatimaye alikabidhi kitita cha shilingi milioni 10 mzee huyo.

Baada ya kupokezwa hela hizo Mzee Makosa alisema kuwa msanii huyo alimfanyia kitu ambacho hakijawai kufanywa kwa ajili yake.

“Mimi sina maneno mengi, kwa sababu cha kusema kuhusu Diamond sikioni kikija kichwani. Alichokifanya alichokifikiri ni yeye. Kafanya kitu ambacho watu wengi hawajafanya. Basi nibaki tu kumshukuru yeye na kuwashukuru wanaomuunga mkono katika harakati zake.”   Alisema Mzee Makosa katika mahojiano na kituo cha redio cha Wasafi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved