Katika TikTok alipoenda Live, Musila ambaye alionekana akijivinjari kwa nyimbo za mumewe aliwafokea kwa ukali watu ambao wanaeneza chuki dhidi yake mtandaoni.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 54 alisema mpaka sasa hajawahi elewa kwa nini watu wanaumia sana yeye kuolewa na Guardian Angel mwenye umri wa miaka 34.
Alisema kuwa hata wanaomuita mzee pengine huenda hawataishi miaka ambayo ameishi na kuwakumbusha kuwa uzee ungalipo na wao watazeeka pia wakati mmoja.
“Unajua hawa watu ambao huwa wananiita ‘mzee’ yaani hawashangaa. Wewe ni chuma ya Doshi hutawahi zeeka ama nini? Anyway baadhi yenu mtakufa mkiwa wadogo hivyo nawaelewa,” Musila alisema huku akimtabasamia mume wake.
Mwingine alimwambia kwamba hawezi badilisha ukweli uliopo kuwa Guardian Angel ni mdogo na Musila akamjibu kwamba anajuaje ni mdogo wake yeye ni mwanamume tayari.
Musila alisema kwamba maisha ni mafupi sana na yeye hufanya kadri ya uwezo wake kufurahia kila sekunde ya uhai wake.
“Unajua maisha ni mafupi sana, wakati ninaangalia katika maisha, miaka 54 na ninaona baadhi ya watu wenye chuki eti nimekuwa mzee, pole kwenu. Yaani kama mtafika hiyo miaka, mtakuwa mnateseka sana,” aliongeza.
“Umri ni neema na ndio maana sijawahi fika miaka yangu. Ningetaka ningeficha umri wangu lakini mimi ni mmoja kati ya wachache ambao tunajivunia umri wetu kwa sababu na umri wangu huu Mungu ameni9bariki sana,’ aliongeza.
Aliwakemea wanaomtukana akisema kuwa kama wao ni warembo kumliko mbona Guardian Angel hakuwaona na kuwaoa badala yake.
“Mimi ni mzee lakini niko fine. Hao mnanitukana hapa, mbona bwanangu hakuwaona?” aliuliza.