Mrembo Edday Nderitu amezua mjadala pevu kwenye mtandao wa Facebook baada ya kupachika picha akiwa katika hali ya furaha na mpenziwe, Samidoh.
Wawili hao walijumuika pamoja kwa mara nyingine nchini Marekani ambapo Edday alimkwamilia Samidoh kifuani na kumsherehekea kwa ujumbe mtamu.
Samidoh alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na vEdday hakucheleaq kuonyesha jinsi alivyo mtu wa maana katika maisha yake licha ya kuwepo kwa misukosuko kwenye ndoa yao katika miaka ya hivi karibuni.
Akiwa kifuani mwa Samidoh na tabasamu tele, Edday alimsherehekea kama mpenzi na baba wa ajabu kwa wanao na kuonyesha shukrani kwa kila wakati mzuri wanaoshiriki pamoja.
“Heri ya Siku ya Kuzaliwa kwa rafiki yangu, mshirika, na baba wa ajabu kwa watoto wetu. Uwepo wako unamaanisha mengi, na tunashukuru kwa kila wakati unaoshirikiwa. Ubarikiwe na miaka mingi zaidi ya afya, furaha, na upendo. Hapa kuna maisha marefu, yenye kuridhisha mbeleni!” Edday aliandika.
Picha na ujumbe huu vinajiri wakati ambapo wengi walishashawishika muda mrefu kwamba wawili hao hawawawezi kupatana tena kutokana na mifarakano ya mara kwa mara baada ya ujio wa penzi la tatu – Karen Nyamu.
Mwaka jana, Edday alimpasha Samidoh vikali mtandaoni baada ya kuondoka nchini na wanawe kuelekea USA na kusema kwamba ilimbidi apige breki safari ya miaka 15 ya ndoa yake na Samidoh baada ya msanii huyo kuonyesha wazi kwamba anampenda pia Karen Nyamu.
Edday aliweka wazi kwamba ilimbidi andoke kwa kile alichokijata kuwa ni kutokuwa tayari kuishi katika ndoa ya wanawake wengi.
Ikumbukwe Samidoh na Edday Nderitu wana watoto 3 pamoja huku msanii huyo akipata watoto wengine 2 na seneta Karen Nyamu, jambo lililozua nyufa kwenye penzi lake na Edday.
Hata hivyo, wanasema watu wqawili ambao wameshiriki maisha yao kwenye kitanda kimoja katu vusiyaingilie, na kweli kwa kauli hiyo, ni wazi kwamba Edday na Samidoh wamerejesha uhusiano wao mzuri.
Hii si mara ya kwanza kwa Samidoh kukutana na Edday nchini Marekani, kila mara anapozuru taifa hilo kwa shughuli zake za kimuziki, licha ya Edday kunukuliwa akisema kwa hasira kwamba angehakikisha Samidoh hakutani na wanawe hata kidogo.