logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Vybz Kartel amvisha pete ya uchumba mpenziwe aliyemsubiri kipindi chote akiwa jela

"Ulikuwepo wakati nilikuhitaji sana, na sitakuacha kamwe, mpenzi. Ninathamini kila ziara, kila simu, na nyakati zote tulizotumia kuzungumza, kucheka, na hata kulia pamoja.”

image
na MOSES SAGWE

Burudani06 November 2024 - 12:04

Muhtasari


  • “Umekuwa mwamba wangu, rafiki yangu bora, na mwandamani wangu. Naomba tukae pamoja kwa muda wote ninaoishi. Ninakupenda, mpenzi."
  • Wanandoa hao walikutana kwa mara ya kwanza mnamo 2015 wakati Kartel alikuwa akitumikia kifungo kufuatia hukumu ya mauaji. 



Mkali wa Dancehall Vybz Kartel amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi, Sidem Öztürk.

Msanii huyo alitoa tangazo hilo la dhati katika video iliyoshirikiwa kwenye Instagram Jumanne.

Kartel alifichua kwamba Sidem amekwama naye katika penzi la dhati tangu akiwa gerezani na njia pekee ya kulipa wema na fadhili zake ni kwa kuitangazia dunia kuwa bado anampenda.

"Ni rasmi ... nilikuvisha pete nikiwa gerezani, lakini pia nimekuvisha pete katika maisha halisi," Kartel aliandika kwenye maelezo ya kihisia.

"Ulikuwepo wakati nilikuhitaji sana, na sitakuacha kamwe, mpenzi. Ninathamini kila ziara, kila simu, na nyakati zote tulizotumia kuzungumza, kucheka, na hata kulia pamoja.”


“Umekuwa mwamba wangu, rafiki yangu bora, na mwandamani wangu. Naomba tukae pamoja kwa muda wote ninaoishi. Ninakupenda, mpenzi."


Wanandoa hao walikutana kwa mara ya kwanza mnamo 2015 wakati Kartel alikuwa akitumikia kifungo kufuatia hukumu ya mauaji.

Katika mahojiano ya awali, wawili hao wamezungumza kuhusu safari yao na kujitolea kwao kwa miaka mingi hadi kuachiliwa kwa Kartel kutoka gerezani Julai, baada ya hukumu yake kubatilishwa.

Tangu wakati huo wamezindua chaneli yao ya YouTube, Kiss Me Baby, ambapo wanashiriki muhtasari wa maisha yao ya kila siku na kutoa uangalizi wa karibu zaidi wa hadithi yao ya mapenzi.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved