logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mchungaji aliyetabiri ushindi wa Kamala Harris ashindwa kujitetea baada ya video hiyo kuibuliwa

Mchungaji Suleiman kwa madaha, alisimama kwenye mimbari takatifu na kuwadanganya wuamini kwamba Mungu amemnenea katika ndoto kuwa Harris atamshinda Trump kwa kura nyingi ajabu.

image
na MOSES SAGWE

Burudani07 November 2024 - 15:58

Muhtasari


  • Baada ya hali halisi kutimia, watu katika mitandao ya kijamii wamemkabili vikali mchungaji huyo kujieleza ni wapi utabiri wake ulikwenda fyongo.
  • Mchungaji huyo ametoweka mitandaoni bila kuzungumza chochote kuhusu uchaguzi wa Marekani ambao ulifuatiliwa zaidi barani Afrika.




Mchungaji mmoja wa Kiafrika aliyetabiri kuwa naibu rais wa zamani wa Marekani Kamala Harris angeshinda uchaguzi wa urais na kuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais katika taifa hilo, ameshindwa pa kuficha aibu yake baada ya Trump kuibuka mshindi.


Mchungaji maarufu wa Nigeria, Apostle Johnson Suleman alirekodiwa miezi michache iliyopita akitabiri kuwa Mungu amempa maono na ufunuo kwamba Marekani itapata rais wa kwanza mwanamke katika historia yao.


Hii ni baada ya chama cha Democrats kumkabidhi Harris tikiti ya kumenyana na Trump wa Republican, baada ya rais Joe Biden kushinikizwa hadi kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.


Mchungaji Suleiman kwa madaha, alisimama kwenye mimbari takatifu na kuwadanganya wuamini kwamba Mungu amemnenea katika ndoto kuwa Harris atamshinda Trump kwa kura nyingi ajabu.


Mtume Suleman, mwinjilisti wa televisheni na mchungaji mkuu na mwangalizi mkuu wa Omega Fire Ministries International katika video ya unabii alipokuwa akizungumza na waumini wake aliwathibitishia kuwa Kamala Harris atashinda uchaguzi wa Marekani, akidai kuwa Mungu alisema naye.


 


Akiongea zaidi, Mtume Suleman anawaambia wasikilizaji wake waandike kwani anaamini sana alichoambiwa na Mungu wake kuwa Makamu wa Rais Kamala Haris atamshinda Donald Trump wakati wa uchaguzi.


Hata hivyo, mwisho wa siku, utabiri wa mtume Suleman ulikosea kabisa huku rais wa zamani Donald Trump akishinda uchaguzi wa Marekani dhidi ya Kamala Harris.


 


Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump alipita kwa raha kura 270 za uchaguzi zinazohitajika kushinda Ikulu ya White House, na kupata kura 292, huku Mdemokrat Kamala Harris akipata 224.


Baada ya hali halisi kutimia, watu katika mitandao ya kijamii wamemkabili vikali mchungaji huyo kujieleza ni wapi utabiri wake ulikwenda fyongo.


Mchungaji huyo ametoweka mitandaoni bila kuzungumza chochote kuhusu uchaguzi wa Marekani ambao ulifuatiliwa zaidi barani Afrika.


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved