Siku ya Ijumaa, mtangazaji maarufu wa runinga Betty Mutei Kyallo na mpenzi wake wa miaka 26 Charlie Jones waliadhimisha mwaka mmoja wa uhusiano wao.
Wapenzi hao wawili waliadhimisha siku hiyo maalum kwa kusherehekeana na kupeana shukran kwa safari yao ya mapenzi katika mwaka mmoja uliopita.
Charlie alisema kuwa siku ambayo alikutana na Betty mwaka mmoja uliopita ilikuwa siku bora zaidi maishani mwake na akabainisha kwamba sasa wako pamoja daima.
Aidha, alimsherehekea mtangazaji huyo mrembo wa Runinga kwa majina mengi maalum na akabainisha kuwa aliathiri maisha yake vyema walipokutana.
"Mwaka mmoja uliopita leo sikujua ningepata mke, rafiki mkubwa, mchumba, amani yangu, furaha yangu, nguvu, na mambo mengi, orodha hiyo haina kikomo kutoka kwa Betty Kyallo," Charlie alisema.
Aliongeza, "Tuliweka msingi ambao hakuna mtu anayeweza kuvunja, maisha ya baadaye, na familia. Ulinifungua bora zaidi yangu."
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 aliendelea kuzungumziamipangomikubwa ya siku za usoni kwa mama huyo wa binti mmoja akisema mwaka wao wa kwanza ulikuwa msingi tu.
"Awamu inayofuata ni kupata kila kitu unachostahili. Ya kwanza ilikuwa msingi, inayofuata ni maisha ya kifalme. Nilikupata maishani,” alisema.
Pia alifichua jinsi mtangazaji huyo alivyomfanya abadili staili yake ya nywele walipoanza kuchumbiana.
Betty kwa upande wake alionekana kuthamini ujumbe mzuri wa mpenzi wake na pia akaonyesha kumbukumbu zao nzuri.
Wawili hao walifichua uhusiano wao mapema mwaka huu, na kumaliza uvumi ambao ulikuwa kwenye mitandao ya kijamii kwa muda.
Hata hivyo walilazimika kupambana na ukosoaji mwingi mtandaoni huku wengi wakizungumza kuhusu tofauti zao za umri. Betty ni mkubwa kiumri kwa miaka kadhaa kuliko mpenzi.