Msanii nguli wa muziki wa Rap kutoka Marekani Marshall Bruce Mathers maarufu kama Eminem amempoteza mama mzazi.
Kifo cha Debbie Nelson, kutoka Missouri kilithibitiwa na mwakilishi ambaye pia ni msaidizi wa muda mrefu wa Eminem Dennis Dennehey ijapokuwa kwenye ujumbe wake hakutaja chanzo cha kifo cha Bi Nelson.
Deborah Rae Nelson alizaliwa mnamo Januari 6 mwaka wa 1955 kwa wazazi Betty Hixson na Bob Nelson. Wazazi wa Eminem walifanya kazi pamoja na kuimba katika kundi lililoitwa ‘’Daddy Warbucks’’ na baadaye kuoana wakiwa na umri wa ujana. na umri wa miaka 17, Debbie Nelson alimzaa mtoto wake wa kwanza kwa jina Marshall anayefahamika kwa jina la usanii kama Eminem mnamo Octoba 17, 1972.
Bi Nelson na Mather walitalikiana baadaye huku mtoto wao Marshall akiwa mchanga. Baadaye uhusiano baiana ya wazazi wa Eminem ulitajwa kuwa na dosari iliyopelekea kuvunjika kwa ndoa yao kupitia talaka. Wakati mmoja, Eminem alikiri kwamba katika umri wake mdogo akianza usanii mamake alimtekeleza kwa kutowajibika katika malezi akidai kuwa alikuwa akimpiga na kumtusi.
Baadaye Bi Nelson alimshtaki mwanawe Marshall ‘Eminem’ kwa kashfa ya kumchafulia jina mnamo mwaka wa 1999. Hata hivyo wawili hao kwa muda mrefu wamejaribu kupatana.
Eminem alitoa albamu mwaka wa 2013, iliyoitwa ‘’Headlights’’ ambayo ilileta mabadiliko katika uhusiano wao kwani alionyesha kujuta kwa maneno makali aliyotumia dhidi ya mama yake na kumwomba msamaha kutokana na uhusiano wao mbaya.
Hata hivyo uhusiano baina ya wawili hao ulionekana kuimarika baada ya Eminem kuwachilia albamu nyingine mwaka wa 2022 baada yai Bi Nelson Debbie kumpongeza.
Bi Nelson alifariki Jumatatu usiku akiwa na umri wa miaka 69.