logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Zuchu Apuuzilia Mbali Dhana Ya Ushetani Katika Muonekano Wake Kwenye Video Mpya

“Kwa wale wanaonijua watakuambia ile ni video tu. Mimi nampenda Mungu kuliko kitu kingine chochote, hata sijui kama hicho kitu kinachoitwa ‘iluminati’ ni cha kweli.”

image
na MOSES SAGWE

Burudani08 December 2024 - 15:47

Muhtasari


  • Lakini Zuchu si wa kwanza kujikuta kwenye kikaango cha mashabiki kutokana na muonekano kwenye video yake.
  • Mwaka jana, msanii wa Nigeria, Rema alizua mjadala mkali mitandaoni baada ya kutoa picha na video zenye muonekano ambao uliwakanganya mashabiki wake wengi.



KWA mara ya kwanza baada ya kuachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Antennae’, msanii Zuchu amezungumzia ubunifu alioutumia kwenye video ile.


Akizungumza na waandishi wa Habari za burudani katika angatua ya JKIA baada ya kuwasili kwa ajili ya shoo yake nchini Kenya Jumamosi, Zuchu aliulizwa kuhusu ubunifu huo ambao kwa wengi umeeleweka kuwa si wa kawaida.


Baadhi ya watu ambao wameitazama video hiyo walihisi kwamba ubunifu wa Zuchu kutokea akiwa na vazi lisolo la kawaida ambalo linatoa picha ya kishirikina vile na alitakiwa kunyoosha maelezo kuhusu mtazamo huo.


Zuchu alikanusha uhusiano wowote na nguvu za giza akisema kwamba wale wanaomjua kwa undani watamwambia mtu yeyote wakati wowote kwamba huo ni uigizaji tu na hamna lingine zaidi.


“Kwa wale wanaonijua watakuambia ile ni video tu. Mimi nampenda Mungu kuliko kitu kingine chochote, hata sijui kama hicho kitu kinachoitwa ‘iluminati’ ni cha kweli.”


“Ile ilikuwa acting tu, nilitaka tu kuwa na kitu kipya kabisa wakati nafanya video nikiimba, hivyo tu,” Mrembo huyo alijieleza kwa maelezo ya kina.


Zuchu aliandamana na Diamond kwa ajili ya shoo ya Furaha Fest ambayo ilifanyika Jumamosi jijini Nairobi.


Lakini Zuchu si wa kwanza kujikuta kwenye kikaango cha mashabiki kutokana na muonekano kwenye video yake.


Mwaka jana, msanii wa Nigeria, Rema alizua mjadala mkali mitandaoni baada ya kutoa picha na video zenye muonekano ambao uliwakanganya mashabiki wake wengi.


Uvumi huo ulimlazimu Rema kunyoosha maelezo naye akisema tu kwamba hamna dhana yoyote zaidi ya ubunifu tu.


Rema aliandika, “RAVAGE UPRISING/ Shaba za Wahenga Wangu hukaa kwenye jumba la makumbusho la jiji hili hili, kwa hivyo nilitengeneza yangu upya. Kwa hivyo, Edo amefafanuliwa upya, ramani imeundwa upya, akili zako zimeamshwa na kinyago kuzaliwa upya. Asante London! 🦇🇬🇧”


Awali, shoo yake iliyotarajiwa kufanyika nchini Ethiopia ilifutiliwa mbali kwa kile tetesi zilisema kuwa ni utata uliozunguka mkufu wake wa shingoni.


Mkufu huo ulidaiwa kuwa na mchoro wa kanisa linalochomeka lakini pia misalaba iliyopinduliwa juu-chini.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved