HATIMAYE, mrembo Georgina Njenga amemtambulisha
mpenzi mpya, ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja baada ya uhusiano wake wa awali
kusambaratika.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Georgina Njenga
alichapisha msururu wa picha akiwa na mpenzi mpya.
Mama huyo wa mtoto mmoja, binti, alifuatisha picha
hizo na ujumbe wa kimahaba akimtaja kijana huyo mwenye habati kama mfalme wa
himaya ya moyo wake. Akionesha ukaribu wao ulivyokolea, Njenga aliweka wazi
kwamba kumbukumbu nzuri ya mwaka huu kwake ni kumpata yeye.
“Hey
mpenzi wangu, kumbukumbu pendwa kwangu mwaka huu imekuwa kukutana na wewe. Wewe
ndiye kitu kizuri kuwahi kutokea kwangu na kusema kweli hatimaye kusema nina
mtu wa kupenda ni hatua kubwa nwangu,” Georgina Njenga
alisema.
“Nakupenda
sana mpenzi wangu na shukrani kwa kunielewa kwa kina ambacho hakuna yeyote
amewahi kuelewa. Kwa kweli, wewe umetumwa kutoka kwa Mungu mpenzi wangu,”
Georgina aliongeza.
Mwaka jana mwezi Julai, Georgina Njenga na baba binti
yake, Tyler Mbaya maarufu kama Baha Machachari walitangaza kuachana baada ya
penzi lao kudumu kwa miaka michache.
Kuachana kwao kulijiri wiki chache baada ya Baha
kudaiwa kuingia katika uraibu wa Kamari za mitandaoni.
Hata hivyo, Georgina Njenga mwezi Februari mwaka huu
katika mahojiano, alifunguka kwa kina akielezea kiini cha penzi lao kuvunjika.
Akiongea kwenye mahojiano na SPM Buzz, Georgina
alifichua kuwa sababu kubwa iliyomfanya aachane na Tyler ni kwa sababu wote
wawili walikuwa na malengo tofauti, jambo lililowafanya waone ni bora waachane,
na kuongeza kuwa uhusiano wao haukuwa na mafanikio hata kidogo.
“Katika
mahusiano, maeneo ya Inafika, kila mmoja wenu ana malengo tofauti… nilikuwa na
malengo tofauti; alikuwa na malengo tofauti, na hatukuweza kufikia malengo yetu
kwa njia moja ...Mambo mengi ya kibinafsi hayakuwa yakifanya kazi, ambayo
nisingependa kuyazungumzia hapa,” Georgina alishiriki.
Mama wa mtoto mmoja alishiriki zaidi maoni yake juu ya
kuokoa uhusiano akikushauri zaidi ikiwa umejaribu kuongea na bado haifanyi
kazi, ni sawa sana kuondoka, kwani huna haki.
"Binafsi,
siamini kila kitu kinapaswa kuwa milele. Ikiwa haifanyi kazi na ninyi
mmejaribu, mnaweza kuiacha iende, "Georgina alishiriki.