logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Gold Scams Na Wash Wash Sio Njia Yangu” – Kennedy Rapudo Ajibu Madai

“Hata hivyo, wakati nilikuwa maskini miaka ya nyuma, hakuna aliyethubutu kufuatilia chanzo cha umaskini wangu. Ama tuseme ni wivu, njaa na roho chafu?” alihoji.

image
na MOSES SAGWE

Burudani06 January 2025 - 09:57

Muhtasari


  • “Hata hivyo, wakati nilikuwa maskini miaka ya nyuma, hakuna aliyethubutu kufuatilia chanzo cha umaskini wangu. Ama tuseme ni wivu, njaa na roho chafu?” alihoji.
  • Alisema kwamba kila mtu kwa sasa anafaa kuelekeza nguvu zake kwa kukosoa uongozi mbaya wa serikali na si katika kupoteza usingizi kwa utajiri wa mtu binafsi.



KENNEDY RAPUDO, mume tajiri wa mwanasosholaiti Amber Ray kwa mara nyingine tena amekanusha madai ya kuhusishwa na biashara haramu ya kutakatisha fedha na kughushi dhahabu.


Kupitia kwa taarifa ndefu kwenye ukurasa wake wa Instagram, Rapudo alisisiti9za kwamba biasara ya kutakatisha fedha na kuuza dhahabu bandia sio njia yake na wala haitokuja kutokea kuwa biashara yake.


Rapudo ambaye ni tajiri msiri kuhusu chanzo cha utajiri wake alisema kwamba wachache ambao wanamfahamu vizuri wanaweza toa ithibati kuwa utajiri wake ni halali.


“Utapeli wa dhahabu? Utakatisaji wa fedha? Hizo sio njia zangu na haziwezi kuwa njia zangu. Ukweli ni kwamba watu ambao wananijua kiukweli wanaelewa maadili na kanuni zangu. Sijawai jihusisha katika kitu chochote haramu,” Rapudo alithibitisha.


Rapudo alisema kuwa kama wale wanaofuatilia Habari za biashara hizo haramu wanataka kupata ukweli, basi wanaweza pata majibu kutoka kwa idara husika kama vile DCI.


Tajiri huyo alisema kwamba kwa vile aliamua kuweka maisha yake faraghani na kuficha vyanzo vya utajiri wake haimaanishi kwamba ni haramu.


“Kwa vile mtu aliamua kuishi maisha ya faragha na kutanika vyanzo vya utajiri wake haina maana kwamba wanajihusisha katika biashara haramu. Inasikitisha sana kuona jinsi watu wameamua kujikita katika kufuatilia mambo ya watu badala ya kuzingatia maisha yao.”


“Wakati wanaongea, nitaendelea kusonga mbele, kujenga maisha yangu kwa njia sahihi, njia moja ya kweli kwa kila hatua,” Rapudo aliongeza.


Rapudo alisema kuwa wakati alikuwa maskini miaka ya nyuma, hakuna ata mtu mmoja aliyefanya uthubutu wa kufuatilia chanzo cha utajiri wake, lakini sasa kwa vile anavyo, kila mtu yuko na uchu wa kutaka kujua.


“Hata hivyo, wakati nilikuwa maskini miaka ya nyuma, hakuna aliyethubutu kufuatilia chanzo cha umaskini wangu. Ama tuseme ni wivu, njaa na roho chafu?” alihoji.


Alisema kwamba kila mtu kwa sasa anafaa kuelekeza nguvu zake kwa kukosoa uongozi mbaya wa serikali na si katika kupoteza usingizi kwa utajiri wa mtu binafsi.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved