RAPA STEVO Simple Boy amefunguka kwa undani kiini cha ziara yake ya takribani wiki moja nchini Tanzania mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza kwenye mahojiano na mwanablogu Trudy
Kitui, Stevo Simple Boy alifichua kwamba ziara yake haikuwa ya kujivinjari bali
ilikuwa ya kufuatilia miadi ya kikazi.
Msanii huyo aliyesafiri na meneja wake Machabe
alisema kwamba alikuwa anafuatilia ahadi ya kolabo na moja kati ya wasanii
wanaofanya vizuri kutoka nchini humo, Harmonize.
Alisema kwamba alihisi Harmonize alivutiwa na ngoma
yake ya ‘Inauma lakini itabidi umezoea’ aliyoifanya miaka ya nyumba baada ya
kumuona bosi huyo wa lebo ya Konde Music Worldwide akiimba kipande chake.
Hivyo alifunga safari kufuatilia kama angeweza
kufanikisha kolabo hiyo, jambo ambalo alisema kwa bahati mbaya halikufaulu.
“Tanzania
nilikuwa nimeenda kutafuta Harmonize na Simba (Diamond Platnumz). Kwa bahati
mbaya sikukutana na wao kwa sababu muda wetu na wao haukuoana. Lengo langu
lilikuwa, kama naweza kurudisha nyumba kitambo kidogo, kuna wakati ile ngoma
yangu ‘inauma but itabidi tuzoee’ Harmonize aliimba kipande kifupi…”
“…na
wakati alikuwa hapa Kenya akapigia simu meneja wangu wa kitambo akisema
angetaka kufanya kazi na mimi. Lakini vitu havikuenda sawa, hivyo nilikuwa
nimeenda kumtafuta huko angalau tufanye hata kolabo moja. Kwa bahati mbaya
hatukuweza kukutana lakini huu mwaka nafikiri itatimia,”
Stevo alieleza.