logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chief Godlove Adai Hawezi Safiri Nje Ya Tz Sababu Hakuna Atakayeachia Nyoka Wake

Godlove alisema kwamba hawezi kusafiri kuenda Dubai na Marekani kujivinjari kama matajiri wenzake, kwa vile hakuna mtu atakayeachia nyoka wake kumlisha.

image
na MOSES SAGWE

Burudani11 January 2025 - 08:56

Muhtasari


  • Mwaka 2025 ulipoanza, Chief Godlove alisema kwamba ombi lake kuu mwaka huu ni Mungu kumwepushia wanawake wasiopenda hela kwani watamfanya kuwa mzembe wa kuzitafuta.

CHIEF GODLOVE Mwakibete, kijana mdogo mwenye utajiri wa kushangaza kutoka nchini Tanzania ameibuka na mapya akiwajibu mbona mara nyingi huwa hasafiri nje ya nchi.


Kijana huyo ambaye ameibukia kuwa gumzo kubwa mitandaoni miezi ya hivi karibuni kutokana na utajiri wake, alisema kwamba amekuwa akipata maswali mengi kutoka kwa watu wanaohoji mbona huwa hasafiri kwenda kula bata katika mataifa na miji ya kitajiri kama vile Dubai na Marekani kama matajiri wenzake.


Akijibu swali hilo kwa utani, Godlove alisema kwamba hawezi kusafiri kuenda Dubai na Marekani kujivinjari kama matajiri wenzake, kwa vile hakuna mtu atakayeachia nyoka wake kumlisha.


“Mnaouliza mbona siendi Dubai na Marekani, nyoka mtalisha nyinyi? Kwendeni zenu, siendi Marekani wala Dubai, majini yangu na mizimu atalisha nani?” Godlove alijibu kwa utani usio wa kawaida.


Hata hivyo, kijana huyo alifuta chapisho hilo baadae kutoka kwenye kurasa zake za Instagram na X alikokuwa amezichapisha siku ya Alhamisi.



Jibu hilo, japo lilikuwa la kitani, lakini lilionekana kuzua maswali mengi kuliko majibu miongoni mwa watu anaowatia moyo katika safari ya kutafuta utajiri.


Hii si mara ya kwanza kwa mkwasi huyo mchanga kutoa kauli za kutatanisha kuhusu Imani yake katika utajiri na Uuungu.


Siku chache zilizopita, Godlove alionekana kutilia shaka uwepo wa mbinguni, akisema kwamba viongozi wa kidini wanaotangaza Habari za mbinguni hata wao wenyewe hawaijui.


“Ukitaka Habari za kwenda mbinguni hata anaekusisimulia Habari za huko ajawahi kwenda fuatilia wachungaji na mashekhe ukitaka kujitambua wewe ninani umezaliwa kufanya nini ili ufanikiwe Kua na uwezo wa kujitibu na kujiombea nisikilize kisha fuata nnachokuelekeza mimi,” Godlove aliandika kwenye X, Januari 3.


Mwaka 2025 ulipoanza, Chief Godlove alisema kwamba ombi lake kuu mwaka huu ni Mungu kumwepushia wanawake wasiopenda hela kwani watamfanya kuwa mzembe wa kuzitafuta.


“Mwaka 2025 mungu niepushie wanawake wasiopenda pesa watanifanya niwe maskini,” aliomba.


Katika


Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved