logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Drake aondoa hatua za kisheria kuhusu diss-track ya Kendrick Lamar (Not Like Us)

Drake amaliza kesi aliyoshtaki Universal Music Group na Spotify kisa diss track ya Lamar

image
na OTIENO TONNY

Burudani16 January 2025 - 10:05

Muhtasari


  • Mwimbaji huyo  alishutumu kampuni hizo kushirikiana kupunguza viwango vya leseni za utiririshaji kwenye diss track ya Kendrick.
  • Wasimamizi wa Kampuni hiyo ya UMG  walisema katika ujumbe wao kuwa pendekezo kwamba UMG itafanya chochote kudhalilisha  na kupaka tope  msanii wake yeyote ni ya kukera na sio kweli.


Drake ameondoa ombi la kisheria alilowasilisha dhidi ya lebo yake, Universal Music Group (UMG) na Spotify kuhusu wimbo uliovunja rekodi wa Kendrick Lamar ‘Not Like Us.

Nyota huyo wa Canada alichukua hatua Novemba mwaka jana, akidai kuwa kampuni hizo za muziki zilitumia bots, payola na mbinu nyingine kutangaza wimbo wa Lamar ikiwa ni pamoja na kutumia  tabia isiyo halali ya kulipa kituo cha redio cha kibiashara kucheza wimbo bila kituo hicho kufichua malipo hayo,  ambao ulimshutumu kuwa paedophilia.

Mwimbaji huyo  alishutumu kampuni hizo kushirikiana kupunguza viwango vya leseni za utiririshaji kwenye diss track ya Kendrick.

‘’Uenezaji wa ngoma hiyo iliyovunja rekodi ‘’Not like us’’ kwenye utiririshaji , mauzo na uchezaji wa redio ulifanywa kimakusudi na unaonekana kutegemea mazoea ya kibiashara yasiyo ya kawaida na yasiyofaa,’’ Hii ni kutokana na ujumbe ulioandikiwa mahakama.

Wasimamizi wa Kampuni hiyo ya UMG  walisema katika ujumbe wao kuwa pendekezo kwamba UMG itafanya chochote kudhalilisha  na kupaka tope  msanii wake yeyote ni ya kukera na sio kweli.

‘’Pendekezo kwamba UMG itafanya chochote kudunisha msanii wake yeyote ni jambo la kukera na si kweli na kuongeza, Tunatumia kanuni za maadili ya hali ya juu katika kampeni zetu za uuzaji na utangazaji. Hakuna kiasi cha hoja za kisheria za kubuni na za kipuuzi katika uwasilishaji huu wa kabla ya hatua unaweza inaficha ukweli kwamba mashabiki wanachagua muziki wanaotaka kusikia."

Siku ya Jumanne, mawakili wa Drake kwa hiari yao waliondoa kesi ya awali dhidi ya UMG na Spotify, na hivyo kumaliza kesi hiyo.

Hati za mahakama ya New York zilizoonwa na Rolling Stone  zilisoma kuwa ‘’mlalamishi anaacha kesi hii maaalum kwa hiari kwa wajibu wote bila gharama kwa upande wowote’’

Hapo awali Drake aliwasilisha ombi lingine huko Texas, akidai UMG ililipa kundi la redio la iHeartRadio kucheza 'Not Like Us', na kwamba UMG iliruhusu kuachiliwa kwa wimbo huo licha ya kujua kuwa ulikuwa na tuhuma za Drake kuwa "certified paedophile." Ombi hili linabaki kuwa amilifu.

Wimbo huo wa ‘Not Like Us ' ilikuwa pigo la mwisho katika mzozo wa muda mrefu kati ya Drake na Lamar, wimbo ambao ulihitimisha vita vyao vya kufoka. Walakini, maoni ya umma yamegeuka zaidi dhidi ya Drake tangu wakati huo.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wameeleza kuwa kesi hiyo ya kisheria ilikuwa na nguvu kwa Drake kujiondoa kwenye dili lake na Universal, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba hakuna aliyewahi kushindwa kwenye vita vya kufoka vibaya hivi na kushitakiwa hapo awali.


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved