SARAH Mtalii, MD wa kampuni ya utalii ya Bonfire Adventures amefichua kwamba aliondoka katika ndoa yake na mapema mwaka 2022.
Akizungumza na Dr Ofweneke kwenye podikasti yake ya
Lessons @30, Sarah alifichua kwamba hisia zake zilihama kabisa kutoka kwa ndoa
na Kabu mapema 2022 japo amekuja kuondoka kabisa kimwili mwishoni mwa 2024.
Alisema kwamba kauli hiyo si geni kwani ni kawaida
kwa wanawake wengi kuondoka katika kitu kihisia mwanzo kabla ya kuondoka
kimwili baadae.
Alikiri kwamba kati ya 2022 na 2024, amekuwa akining’inia
tu katika ndoa yake na Simon Kabu japo kihisia, aliondoka hiyo 2022 mapema.
“Niko
katika amani, na nafikirio unaweza niambia, ninaonekana kama mtu ako na mawazo?
Unajua kwetu sisi wanawake, nimekuja kugundua kwamba tunaondoka kwa ndoa kama
miaka miwili mitatu kabla ya kuja kutoka sasa kimwili,”
Sarah alisema.
“Wanawake
huwa tunaanza kuondoka kiakili, kihisia na mwishoni tunatoka kimwili. Mimi niliondoka
kitambo lakini bado nilikuwa pale. Sijui nasikia watu wakisema nilikuwa tu
nimening’inia ndani pale.”
‘Kihisia
nafikiri naweza kusema niliondoka mapema 2022,’
Sarah aliongeza.
Mjasiriamali huyo alifichua kwamba kitu ambacho
kilikuwa kimemfanya kuning’inia kwa muda huo wote wa zaidi ya miaka miwili ni
watoto lakini pia biashara yao ya Bonfire Adventures.
“Mwanzo
ninaweza sema kwamba watoto walinifanya nikabaki pale kwa muda. Unajua mimi
nimelelewa maisha ya kikamilifu na tamanio langu lilikuwa kuona wanangu
wakikulia maisha kama hayo ambapo kuna mama na baba kwa sababu ninaamini kwamba
kila mzazi ana nafasi yake katika makuzi ya mtoto…”
“…kuna
nafasi ya baba ambayo nilikuwa najua hata nikienda kule nje sitaweza kuijaza,
lakini nimekuja kugundua kwamba ni jambo linawezekana tu,”
alifunguka.
Sarah alisema kwamba kwa sababu biashara yao ilikuwa
katika kasi nzuri, walikuwa wanalazimika kusafiri kujivinjari ambapo wangelala
katika vyumba tofauti.
“Wakati mwingine ningelazimishwa hata kuenda kwa ‘holidays’
ambapo tungelala kwa vyumba tofauti au vyumba pacha,” Sarah alisema akisistiza
kwamba hilo lingefanyika kwa ajili tu ya kibiashara.