MSANII kutoka lebo ya WCB Wasafi Zuchu ameamua kujibu mipigo baada ya baadhi ya wandani kutoka kwa himaya ya Wasafi kuhoji ikiwa bosi wake, Diamond Platnumz ana nia ya dhati ya kufunga ndoa naye.
Ifahamike kwamba kwa zaidi ya miaka 3 sasa, Diamond
na Zuchu wamekuwa wakijidai kuwa mtu na mpenzi wake, licha ya awali kujulikana
kama msanii na bosi wake.
Zuchu aliamua kufungulia mirija yake ya hasira kwa
watangazaji wa Wasafi ambao walikuwa wanajadili redioni kuhusu uwezekano wa
Diamond kumuoa Zuchu hatimaye.
Zogo zima lilianza pale Juma Lokole, mtangazaji
katika kipindi cha Mashamsham alimuuliza Ricardo Momo, kaka wa Diamond kama
kweli Diamond anaweza kumuoa Zuchu.
Lokole katika swali lake alimtaja Zuchu kama king’ang’anizi
anayelazimisha kuolewa na Diamond wakati Diamond mwenyewe anakaa kama hataki vile.
Jambo hili lilionekana kumkera Zuchu ambaye kupitia
Instagram alitoa pofu zito kwa Wasafi akisema kwamba yeye hana haja ya kuolewa
na Diamond na wala hajawahi mshikia bunduki kumtaka ndoa.
“Hebu
naomba nitoe tamko, sina haja wala silazimishi mimi kuolewa na Nasibu
(Diamond). Ifike hatua mtafute vingine vya kuhoji. [Diamond] hana lazima hata
ya kuwa na mimi na sijawahi kumshikia bastola wala kumteka,”
Zuchu alifoka.
“Ana
haki ya kwenda kokote anakoridhika. Maana naona mmeacha kazi mnafanya na sasa
kazi yenu mpya ni kunichafulia chini na kutafuta commwents na likes,”
mrembo huyo aliongeza kwa hasira.
Zuchu aliendelea kubwabwaja katika kile alichokitaja
kama barua ya wazi kwa watangazaji hao akisema kuwa wamekuwa wakitafuta tu
namna yak umuongelelea hata wakati hajafanya lolote la kuzungumziwa.
“Maana
naona huyo Nasibu akiwa na mwanamke dunia nzima inaacha kazi na kuanza
kumuandama. Watu wote, taasisi nzima
kipindi na vipindi vyote ikitokea siku hata mtu iwe birthday yake
mnatafutatu namna mniongelelee,” alisema.
Alimalizia kwa kuwaambia ikiwa wanaona kumng’ang’ania
Diamond ni rahisi kama wanavyosema anamng’ang’ania, basi wako huru kumtafuta
mwanamke wanayetaka wamlete amng’ang’anie Diamond.
“Kama
mnaona ni rahisi sana kumng’ang’ania ambieni hao mnaotaka awe nao wakamng’ang’anie
tuone.”
Mrembo huyo wa malkia wa taarab aliwashauri
watangazaji wa Wasafi kuweka mipaka baina ya kazi yao na mambo yake akisema
kwamba hawammudu hata kidogo.
Zuchu alitishia kuwapeleka Wasafi mahakamani ikiwa
wataendelea kumchokonoa kisa uhusiano wake na bosi wao, Diamond Platnumz.
“Mshauri
[Diaomond] aniache muone kama nitamfuata na mabomu. Wajinga nyinyi hebu
choreeni mipaka, sio kutwa kujifanya mnanimudu. Sasa nasubiri nione, safari hii
nitapeleka mtu mahakamani,” alimaliza.