MUIGIZAJI wa muda mrefu wa filamu za Bongo, Wema Sepetu ametoa kauli ya kujisikitikia akisema kwamba hamu yake ya kuitwa mama imeshatoweka kabisa.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika hafla ya
kisiasa ya chama cha CCM nchini kwao, mrembo huyo ambaye kwa miaka kadhaa
amekuwa akionyesha hamu yake ya kuitwa mama alisema kwamba hana Imani tena kama
atapata mtoto wa kwake.
Wema alisema kwamba kwa umri aliofikia, yeye atabakia
tu ku’adopt mbwa na kuwalea, akisema kwamba yeye anapenda sana mbwa
ikilinganishwa nap aka.
Alisema kwamba hawezi akam’adopt mtoto wa mtu kwa
vile hajui kazaliwa na nani, hivyo anasalia tu kuwalea wanyama kama mbwa.
“Mimi
kuwa na mbwa sioni kama ni kitu cha ajabu sana, mimi ni mpenzi wa mbwa. Sipendi
paka kabisa na siwezi kuacha kupenda mbwa eti kwa sababu watu wanasema napenda
mbwa.”
“Mbwa
wangu Manunu namchukulia kama mtoto wangu, kwa kweli sijafanikiwa kupata mtoto
na kiukweli kwa wakati huu hata mkinifariji kwa maneno ya kunitakia kila la
kheri katika kutafuta mtoto, mimi nimeshafika umri wa miaka 35 sasa na
sitegemei kwamba nitashika mimba tena.”
“Kwa
umri wangu sasa miaka 35, safari yangu ya kutafuta mtoto pia imefika mwisho. Hata
ile hamu haipo, umefika wakati nimekata tamaa,”
Sepetu alisema kwa kujisikitikia.
Alidokeza kwamba ameamua kuishi na ukweli kwamba
hatowai mpakata mwanawe katika mikono yake kwa vile ameshaambiwa ana matatizo
na huo ndio ukweli alioukubali.
“Na
hata ikisemwa kwamba ikitokea sasa hivi… kwanza sidhani kama itatokea kwa
sababu tayari yaani nilishaamua kama nimeshaambiwa bwana wewe una matatizo basi
ishi nayo, na ndio hivyo mwenyezi Mungu ndio kaamua,”
aliongeza.
Alipoulizwa ikiwa ataolewa na mume wake atake mtoto,
Sepetu alisema kwamba ikitokea basi mume wake sharti awe mtu wa kuelewa kwamba
yeye ana shida.
“Kama
atakuwa anajua shida zangu basi itabidi aishi nazo kwa sababu huwezi ukampenda mtu
halafu hukubali shida zake. Ukimpenda mtu mchukue na matatizo yake na mapungufu
yake na kila kitu chake.”
“Mimi
nimeshakubali, nimesema Alhamdulillah kwa sababu nimemtaka [mtoto] kwa muda
mrefu, lakini mwenyezi Mungu akaona kwamba labda sistahili na huwezi kumpinga
Mungu,” Sepetu aliongeza.
Hata hivyo, mrembo huyo alisema kwamba kutopata kwake
mtoto kutamfanya kuwachukia watoto.
“Nitawapenda
watoto wa ndugu na marafiki zangu, huwezi jua kwa nini Mungu kaamua kuninyima
mimi. Ninashukuru Mungu japo inaniuma sana lakini ndio hivyo tena, maisha
yanaenda,’ alimeza mate machungu.