YOUTUBER Diana Marua amezua minong’ono kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kwenye video akimkabili mumewe Bahati Kioko kuhusu ni kwa nini aliacha kumdekeza kwa zawadi.
Wapenzi hao walikuwa wametembelea moja ya mashamba
walioyonunua mwaka jana huko Ngong wakati Diana alimhoji Bahati kwa nini hataki
kumwekea mradi katika shamba hilo ili kumuingizia faida.
Diana alisema kwamba Bahati amekuwa bahili katika siku za
hivi karibuni kiasi kwamba hata hakumbuki ni lini mara ya mwisho alimpa zawadi.
Alimkabili akitaka kujua nini kilibadilika akaacha kumdekeza
kwa zawadi, na kuhoji iwapo mumewe alifilisika.
“Mimi nataka mali kila
mahali, wewe hakikisha tu ninapata mali ndio mwisho wa siku ninatengeneza faida
kutokana na hiyo mali. Sikiliza, umechoka kunitunuku zawadi? Umesota?” Diana alimkabili Bahati.
Bahati kwa kujitetea, alisema kwamba uchumi wa Kenya hauko
vizuri vile na kwamba hakuna mtu ambaye Januari hii ako na pesa.
‘Hakuna mtu ambaye
hajasota sasa hivi, na huu uchumi kuna mtu hajasota kweli?’ Bahati alisema akimjibu
mkewe.
“Hivyo tuseme hutaki kuni’surprise?
Kusema tu ukweli ni lini mara ya mwisho ilini’surprise? Ni lini mara ya mwisho
ulisimamisha Kenya kwa kunizawidi?” Diana alimuuliza tena.
Mama huyo wa watoto 3 alisema kwamba zawadi ya mwisho
alipokea kutoka kwa mumewe ni gari aina ya Range Rover.
“Haujanipa surprise nyingine yoyote. Zawadi ya
mwisho ambayo ilinipa ni Range Rover. Hujanizawidi tena, hujashughulika
tena na mimi…na unajua mimi ni Mjaluo…” Diana alilalamika.
Kwa mujibu wa Diana, angetegemea Bahati angempa bonge la
surprise kama kumweka kwenye mabango makubwa ya barabarani nchini kote.
Alisema kwamba Bahati sawa tu na wanaume wengine,
zawadi ghali na ya maana ambayo

© Radio Jambo 2024. All rights reserved