logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Hii Inauma Sana, Shushu Tafadhali Rudi!" Muigizaji Kate Actress Aomboleza Baada Ya Kufiwa Na Mpendwa

Muigizaji huyo mahiri yuko katika hali ya huzuni baada ya kumpoteza nyanya yake kipenzi.

image
na Samuel Maina

Burudani05 February 2025 - 15:27

Muhtasari


  • Kate alitangaza habari hizo za kusikitisha kupitia akaunti yake ya Instagram siku ya Jumatano, akifichua jinsi alivyoumia sana moyoni.
  • Kate alieleza jinsi alivyoumia moyoni na kumsihi mwanamke huyo aliyempenda sana arudi.

Kate Actress amemuomboleza nyanya yake

Muigizaji mashuhuri wa Kenya Catherine Kamau almaarufu Kate Actress ameingia kwenye maombolezo.

Muigizaji huyo mahiri yuko katika hali ya huzuni baada ya kumpoteza nyanya yake kipenzi.

Alitangaza habari hizo za kusikitisha kupitia akaunti yake ya Instagram siku ya Jumatano, akifichua jinsi alivyoumia sana moyoni.

"Shushu wangu mpendwa!" Kate aliandika kwenye Instastori zake na kuambatanisha taarifa yake na emoji ya moyo uliovunjika na uso wa huzuni.

Mama huyo wa watoto wawili pia alichapisha picha ya kumbukumbu yake na marehemu nyanya yake.

Alieleza jinsi alivyoumia moyoni na kumsihi mwanamke huyo aliyempenda sana arudi.

“Hii inauma sana. Shushu tafadhali rudi,” aliandika.

Kundi la mashabiki na wafuasi wake walimiminika chini ya chapisho lake la huzuni ili kumfariji, na kumtakia nguvu anapoomboleza.

Maureen Kunga: Praying for you my dear. Poleni san.

Luciah Njoki: The Lord is close to the brokenhearted.

Mutahi Kuria: May God comfort you and your loved ones.

Jackie Matubia: Woi pole may she rest in peace.

Kavinya Rose: Pole sana Cate. May Shosh find peace in her rest. My condolences to you and family mama.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved