
MWIMBAJI tajiri wa Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P amemtambulisha mpenzi wake mpya, miaka kadhaa baada ya mahusiano yake baridi na sosholaiti kutoka Cote D’Ivoire, Eudoxie Yao.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Grand P
alichapisha msururu wa picha kadhaa za kimahaba siku ya Ijumaa wakisherehekea
siku ya wapendanao.
Msanii huyo mwenye umbo dogo kimwili alimtambulisha Mrembo huyo
ambaye ana mwili mdogo kama yeye ambaye alimtambulisha kama ‘Mrs Kaba Mariame’
akirejelea jina lake la ukoo.
“Mabawa ya kuku wangu 🥰 tazama jinsi
anavyopendeza 🥰 asante Bwana 🙏 mbaya sana kwa jirani. Bibi
Kaba acha yaliyopita yapite 🙏 Wewe ndiye chanzo cha
furaha yangu, na sitamani chochote zaidi ya kuwa nawe kando yangu maishani.
Njoo karibu na ufariji moyo huu ambao unauliza tu kutetemeka kwa mdundo wa
upendo wako,” Grand P alimbemenda kwa huba.
Kijana huyo amekuwa katika miaka ya nyuma kwenye uhusiano na
sosholaiti wa Ivory Coast Eudoxie Yao ambaye ana umbile kubwa maradufu kumliko
Grand P.
Uhusiano wake na Yao ulionekana kutumbukia mchangani mapema
2023 ambapio kufikia Aprili, alitangaza kuingia katika penzi la mwanadada
mwingine aliyeitwa kwa jina Yubai Zhang.
Grand P alitangaza mahusiano yao kupitia
akaunti yake ya Facebook akithibitisha mapenzi yake na mrembo huyo wa Kiasia na
kuweka wazi kuwa hakuna nafasi ya watu wenye wivu maishani mwao.
"Yubai Zhang wangu, hakuna nafasi kwa
watu wenye wivu," alisema chini ya picha zake na Zhang
alizochapisha Facebook.
Balozi huyo wa Guinea nchini Mali
alikatisha mahusiano yake na mwanamitindo Yao mwaka wa 2021 baada ya kuwa
kwenye mahusiano na mwanamitindo huyo kwa takriban miaka mitatu.
Wawili hao walitangaza kukuwa kwenye
mahusiano ya kimapenzi mwaka wa 2020 baada ya kuchapisha picha wakiwa pamoja.
Mahusiano hayo yaliibua gumzo mitandaoni
kwa ajili ya uzani wao, mashabiki walishangaa ni vipi Grand P mweye mwili mdogo
anaweza kuwa kwenye mahusiano na mwanamke huyo aliyeonekana kumzidi kwa
uzani kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo, haikupita muda mrefu kabla ya
kurudiana na Yao tena katika penzi ambalo lilisuasua kwa muda mrefu hadi
kukamilika mwaka jana tena.