logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wema Sepetu ampa onyo kali tapeli anayetumia jina lake kuwalaghai watu

Wema Sepetu ameonekana kuudhika na tapeli anayetumia maelezo yake kuwatapeli watu kupitia mitandao ya kijamii.

image
na Japheth Nyongesa

Burudani04 March 2025 - 09:10

Muhtasari


  • Sepetu amesikitishwa kwamba licha ya huu kuwa Mwezi mtukufu wa Ramadhani  bado watu wanaendelea kuwalaghai wengine
  • Mwanadada huyo pia ameongeza kwamba kuna  uwezekano laghai huyo ameawalaghai watu wengi sana.

Muigizaji Maarufu nchini Tanzania Wema Sepetu ameonekana kuudhika na tapeli anayetumia maelezo yake kuwatapeli watu kupitia mitandao ya kijamii.

Sepetu ameweka wazi kwamba kuna mtu ambaye anatumia jina lake kuwalaghai watu huku akiwahidi kuwasaidia katika maisha ikiwemo kuwapa kazi pamoja na kuwasaidia kujiunga na kikundi cha waigizaji.

Muigizaji huyo wa bongo amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram huku akiwataka watu kuwa maakini sana na tapeli hao hasa wanaotumia maelezo yanayomuhusu.

Sepetu amesikitishwa kwamba licha ya huu kuwa Mwezi mtukufu wa Ramadhani  bado watu wanaendelea kuwalaghai wengine. Mwanadada huyo pia ameongeza kwamba kuna uwezekano laghai huyo ameawalaghai watu wengi sana.

"Na Ramadhani yote hii bado mtu anatapeli watu na watu wanaingia laini kabisa... Hii imenisikitisha mno... Na sijui mpaka dakika hii kashatapeli wangapi," aliandika Sepetu.

"Jamani hii sio namba yangu ni mtu yupo whatsapp na anatumia info za uwongo kutapaeli watu... Leo kuna rafiki yangu bado kidogo atume 700k kwenye namba hii akiambiwa kuhusu kuchukuwa form za uigizaji na kupewa connection sijui ya kazi... Alieleza Wema Sepetu kupitia maandiko.

Msani huyo wa uigizaji pia aliandika number hio ambayo inatumiwa kuwatapeli wananchi akitaka kutokubali kutuma fedha zozote kwa hiyo nambari au kupena  maelezo yoyote kutoka kwa tapeli huyo.

'*** hii siyo namba yangu... sijui nalipataje hili limutu walahi.." aliendika. 

Swala la utapeli limekekuwa jambo ambalo limekita mizizi katika mataifa mengi ya afrika ikiwemo hapa Kenya. Ni vyema kabisa kuwa maakini sana hasa wakati mtu anaitisha pesa kwa kuahidi msaada au hata mkopo. Ni vizuri kuthibitisha hata kama ni namba ya rafiki yako.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved