
MWAJIRI mmoja amezua mjadala pevu katika mitandao wa X baada ya kufichua moja ya sababu nyingi anazokumbuka zilizomfanya kumnyima kazi mmoja wa watu walioomba nafasi za kufanya kazi kwake.
Katika chapisho hilo, jamaa huyo alifichua kwamba aliwahi
kumfungia nje ya nafasi za ajira mwanamke mmoja kwa kosa la kumpigia simu siku
ya Jumapili.
Kwa mujibu wa mwajiri huyo, msichana huyo alimpigia simu siku
ya Jumapili, jambo ambalo aliona si sahihi kwani lilihitilafiana na umakinifu
wake katika kupokea injili kanisani.
Mtumiaji wa X, aliyetambulika kama @femigibbs, alisema kuwa
simu hiyo ilikatiza muda wake kanisani na ilionyesha vibaya jinsi mgombeaji
huyo wa nafasi ya ajira alikuwa hafai kwa jukumu hilo.
Kwa Maelezo yake, alikuwa amemfanyia msichana huyo mahojiano siku
chache nyuma kwa ajili ya kumwajiri na cha kushangaza akapata Mrembo huyo
akimpigia simu Jumapili hiyo.
"Nilimhoji mtu jana,
alinipigia simu asubuhi ya leo (Jumapili) nikiwa kanisani kuniuliza maswali
ambayo alisahau kuuliza wakati wa mahojiano," aliandika.
Kulingana naye, tayari alikuwa amepanga kumtumia barua ya ofa
kufikia Jumanne lakini akaamua kutofanya hivyo baada ya simu hiyo.
"Wakati wa
mahojiano, utaulizwa ikiwa una maswali yoyote. Huu ndio wakati wa kuuliza
maswali yote ambayo umetayarisha kabla. Ukimwita anayekuhoji baada ya mahojiano
kwa sababu umesahau kuuliza swali, basi inaonyesha kuwa haufai,” aliongeza.
Wengi walisema kuwa kukataa mgombeaji kwa suala dogo kama
hilo hakukuwa sawa na ni dalili ya utamaduni wenye sumu mahali pa kazi.
Mtumiaji wa X @TIOlatunde alijibu, “Watu wengi (sio wanaotafuta kazi
pekee) huwa hawajifunzi maadili ya msingi ya maisha. Inatisha sana. Mjulishe
kuwa huithamini. Ukipenda, tafadhali iruhusu isiathiri ofa yake ya kazi.”
Mtumiaji mwingine @h_abibah alisema, "Wewe ni mtu mbaya
sana, nafasi ndogo usiingie kichwani mwako."
@Tintedeyekay aliongeza, “Hili ndilo tatizo la mashirika ya kuajiri.
Hakuna kutia moyo kwa mawasiliano wazi. Je, alipaswa kukupigia simu wakati wa
saa zako za kibinafsi? Hapana? Je, hii inaweza kusahihishwa wakati wa mchakato
wake wa kupanda ndege? Ndiyo? Unataka kuruhusu matarajio yaende kwa sababu ya
hii?"