
Simba alikuwa anazungumza haya kwenye mahojiano na mwanahabari. Alieza kwamba alikuwa anavutiwa sana na kuwa mwanajeshi baada ya kuwa mwanaskauti kwa siku nyingi na kujifunza mengi.
Wakati akizungumza pia ameweka wazi kwamba wakati alitaka kuwa mwanajeshi hakuwa na tamaa ya kuolewa au kupata mtoto.
"Kipindi niko shule, cha kwanza nilikuwa natamani nije kuwa mwalimu. Baadaye nikaja nikabadilisha mawazo nikasema natakia kuwa mwanajeshi. Nilikuwa na ndoto mbili, kati ya hizo mbili mwenyewe nilikuwa natamani sana kuwa Jeshi," aliweka wazi Mwanamitindo Simba.
"Tulikuwa tunafanya sikauti na nikapewa uwenyekiti na kuna vitu nilikuwa najifunza huko na nikatamni siku moja nije kuwa kamanda. Kidogo ilifika mahali nikaona ni vigumu kuingia jeshi," alieleza.
Akizungumza alifichua kwamba hakuwa na tamaa ya kuolewa wakati akiwa na ndoto ya kuwa mwanajeshi. "Kwa kipindi kile sikuwa na mwawazo ya kuolewa au mawazo ya kuzaa,"
Mwanadada Simba ni mmoja kati ya waigizaji wa kitanzania ambao ndoto yao iling'aa kwa wakati mmoja baada ya kuachilia video ya 'Siri ya Moyo'
Muigizaji huyo kwa sasa ana umri wa miaka 23, ashawahi kuleza kwamba maisha yake ya zamani hayakuwa mazuri hasa baada ya kushindwa kukamilisha masomo yake kutokana na changamoto za karo ya shule.