
PROFESA wa Kijapani ameonya juu ya hali mbaya ya idadi ya watu inayoikabili nchi hiyo ya bara la Asia.
Anadai kuwa, ifikapo mwaka wa 2720, chembechembe za raia wa Japan zitakuwa zimetoweka kabisa duniani, akimaanisha kuwa Japan itakuwa nchi ya kwanza kutoweka kwa njia hii.
Hiroshi Yoshida, Profesa katika Kituo cha Utafiti wa Uchumi
na Jamii ya Wazee cha Chuo Kikuu cha Tohoku, na makadirio yake kwa mwaka wa
2720 ni kwamba Japan itakuwa na mtoto mmoja tu chini ya umri wa miaka 14.
Kama alivyoeleza kwenye jarida la The Times, jeni za
Wajapani zitakoma kuwapo baada ya miaka 695 ijayo.
Takwimu hizi pia zilichapishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani
na Mawasiliano ya Japani mwezi Februari mwaka huu, na kulazimisha serikali
kutafuta suluhu la tatizo hili.
Kati ya 1970, wakati kiwango cha kuzaliwa kilianza kupungua
nchini Japan, na 2005, ni wakati ambapo mabadiliko muhimu yametokea, na vifo
vingi kuliko kuzaliwa.
Mnamo 2022, tayari kulikuwa na vifo karibu milioni moja
zaidi ya waliozaliwa, na 30% ya idadi ya watu zaidi ya miaka 65.
Yoshida anaonyesha kuwa tatizo kubwa ni gharama za maisha
jambo ambalo huwafanya vijana wafikirie mara mbili kabla ya kupata watoto.
Yoshida alifafanua hivi: "Ikiwa kupungua kwa idadi ya
wanaozaliwa haitasimamishwa, 'saa' itarudishwa nyuma," alisema na
kuongeza: "Japani inaweza kuwa nchi ya kwanza kutoweka kutokana na kiwango
cha chini cha kuzaliwa. Tunapaswa kuunda mazingira ambayo wanawake na wazee
wanaweza kufanya kazi na kutamani jamii ambayo kila mtu anashiriki
kikamilifu."
Wanasiasa wengine wanatia hofu zaidi, wakiweka makataa ya
kutafuta suluhu ifikapo 2030.
Kulingana na Newsweek, Japan inapanga kulegeza sera za
uhamiaji nchini humo, hivyo kuruhusu kuwasili kwa watu wapya, ingawa hilo
linaweza pia kumaanisha tatizo.
Wanapanga hata kifurushi cha msaada cha yen trilioni 5.3
kusaidia wanandoa kuanzisha familia.