
MSANII maarufu wa miziki ya Bongo Fleva, Diamond Platnumz amedokeza kuchoshwa na gari lake la kifahari – Rolls Royce.
Kupitia Instagram stories zake, Diamond
alichapisha picha ya gari hilo la kifahari lenye rangi ya samawati na
kufuatisha na ujumbe kwamba amechoka kulitumia na sasa anajiandaa kupokea gari
jingine la kifahari aina ya Bugatti.
Alidokeza kwamba Bugatti limo njiani linasafirishwa
kutoka ughaibuni na pindi litakapofika, utakuwa mwisho wake wa kutumia Rolls
Royce ambalo alinunua takribani miaka 5 iliyopita.
“Nimechoka na hii Rolls Royce,
siwezi ngoja Bugatti langu kuwasili nyumbani,”
Diamond aliandika.
Diamond alionyesha gari hilo kwa mara ya
kwanza mwishoni mwa 2020 likiwa na nambari binafsi ya usajili yenye jina lake,
Platnumz.
Baadae Julai 2021, alibadilisha nambari
hiyo ya usajili na kuweka ‘SIMBA’ katika kile kilichoonekana kama ni kutimiza
ndoto zake za muda mrefu.
Itakumbukwa Wakati fulani mwaka wa 2018
alisema katika mahojino kwamba angelinunua gari hilo ‘hivi karibuni’
Baada ya kulinunua, Diamond aliamsha popo
kwenye Instagram baada ya kuweka kwenye bio yake kwamba ndiye mwanamuziki wa
kwanza kutoka Afrika Mashariki kumiliki gari la Rolls Royce.
Mwaka wa 2016 nyota huo
alionekana katika gari la jeupe la Rolls Royce lakini
baadaye ikagunduliw akwamba alikuwa akifanya video ya wimbo wake
Gari kama hilo lenye gharama
ya juu ni Rolls-Royce Phantom lilimgharimu kati ya $450,000 (
takriban shilingi 45,000,000) kipindi hicho.
Diamond anafahamika kwama
mpenzi wa magari na wakati mwingi huyataja kama ‘my babies’