

MSANII Masauti kutokea Pwani ya Kenya kwa mara nyingine amezungumzia kisa kilichomsibu Mtwapa mwaka jana wakati akitumbuizia mashabiki wake.
Akizungumza katika mahojiano kwenye kituo kimoa cha redio
humu nchini siku chache zilizopita, msanii huyo alirejelea kisa hicho ambapo
alitupiwa nguo ya ndani na shabiki mwanamke wakati anatumbuiza kwenye jukwaa.
Masauti alikiri kwamba lilikuwa ni tukio la kustaajabisha na
la kumpunga vile vile kwani hakuwahi fikiria angefanyiwa kitendo hicho na
shabiki wa kike, akiitaja kama ishara ya mashabiki kumkubali kimuziki.
Katika kisa hicho kilichotokea mwaka jana, Masauti Alifichua kwamba
baada ya kuidaka ile chupi, meneja wake alitaka akabidhiwe lakini Masauti
akakwama nayo kabla ya kuinusa.
“Mwanzo Ilikuwa ni vibe
nilikuwa niko shoo pale yatch watoto wa kike wakapagawa kumuona Masauti. Mtoto Fulani
ambaye mimi sielewi anatokea wapi nashangaa ananirushia jichupi la pink. Nililidaka
mwanzo nikashangaa duh!”
“Halafu meneja si unajua
lazima amlinde msanii, hivyo aliniambia leta hapa, nikamwambia baba eh, hii
nimetupiwa mimi, sasa wewe unataka nikupe kwa mpango gani? Nikamwambia tulia
wacha nicheze nayo hii mpaka nimjue mwenye chupi ni nani,” Masauti alielezea tukio
zima.
Masauti hata hivyo alisema kwamba baadae alikutana na mwenye
kumrushia chupa na ‘kumalizana naye’.
“Chupi nilimrejeshea mwenyewe.
Mwenye chupi tulimalizana,” Masauti alidakia.
Masauti akizungumzia tukio kwa mara ya kwanza mwaka jana,
alisema kwamba hakuwa anatarajia hilo kwani kwa muda mrefu alikuwa anajua
matukio hayo wanafanyiwa wasanii wa nchi za Magharibi na Ulaya.
“Nilirushiwa chupi,
sijawahi kurushiwa chupi kwenye steji ila kwa mara ya kwanza nilirushiwa. Kwa yule
ambaye alirusha bigup sana kwa sababu alinifanya nikajihisi vizuri, unajua video
za kurushiwa chupi tushaziona kwa wasanii kina Drake sijui kina Burna Boy,
halafu sasa mimi hapa Masauti pia nimekuwa msanii wa kwanza Mombasa kurushiwa
chupi,” alisema.
