
MKE mmoja amezua mjadala mtandaoni baada ya kufichua kwamba alimlipisha mumewe zaidi ya dola milioni 3.5 na kuomba gari la kifahari kama zawadi ya kujifungua mtoto wao wa pili.
Alifanya ufichuzi huo katika chapisho lililoshirikiwa kwenye
X (zamani Twitter), akivutia maoni tofauti kwenye mitandao ya kijamii.
Katika chapisho hilo, mwanamke huyo alielezea gharama za
kifahari ambazo mumewe alitarajiwa kulipa - kutoka kwa mitindo ya kifahari hadi
ukarabati wa nyumba - yote yakilenga kumpa binti yao mchanga maisha mazuri na
ya starehe.
Alieleza kwamba baada ya kujifungua, alimshrutisha mumewe
kumpa gari la kifahari aina ya G-Wagon Brabus la rangi ya pink pamoja na pesa
taslimu Sh453,465 kwa matumizi mbalimbali.
Kauli yake: "Mwanzo wa kwanza, G-Wagon ya waridi
iliyopewa nambari ya usajili ya jina langu kama zawadi yangu kwa kumpa mtoto wa
kike, $2 milioni kwenye nyumba mpya, $1 milioni kwa ukarabati na mambo ya
ndani, $100,000 kwenye mifuko minane ya Dior, $80,000 kwenye mkusanyiko mpya wa
Van Cleef, na $10,000 kwa masaji ya kila siku baada ya kujifungua."
Aliendelea kuorodhesha gharama kadhaa zaidi, ambazo zote
ziliripotiwa kufadhiliwa na mumewe baada ya kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili.
Chapisho hilo lilisambaa kwa kasi, na hivyo kuzua hisia
nyingi huku watumiaji wakifurika sehemu ya maoni ili kushiriki maoni yao kuhusu
ishara hiyo ya upendo ya kupindukia.
Tazama video hiyo hapa chini;