
Alicia Kanini, mchezaji na mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali, amezua mjadala miongoni mwa Wakenya kutokana na video yake inayosambaa kwa kasi, na haya ndiyo tunayoyajua kumhusu.
Alicia alizaliwa Machi 31, 2002, na anatoka katika jamii ya Wakamba. Alihudhuria Shule ya Upili ya Wasichana ya Karinga kabla ya kujiunga na Taasisi ya Ufundi ya Kabebe kusomea Stashahada ya Usimamizi wa Biashara.
Kwa mara ya kwanza, Alicia alipata umaarufu kupitia mitindo ya densi zenye nguvu kwenye majukwaa kama TikTok, Instagram, na Facebook.

Alijitokeza kwa kufanya changamoto mbalimbali za densi kwenye TikTok kwa njia ya kudumu, jambo lililomletea wafuasi wengi na upendo mkubwa mtandaoni.
Alipata umaarufu kwa haraka, hasa kupitia TikTok, ambapo alikusanya zaidi ya wafuasi 164,000 na kuvuna zaidi ya milioni moja ya likes.
Baadaye, Alicia aligeukia utayarishaji wa maudhui ya watu wazima, na kujijengea ufuasi mkubwa katika majukwaa kama OnlyFans.
Wakati mmoja, alibadilisha ada ya usajili kwenye akaunti yake kuwa Sh1,300 kwa mwezi, hatua iliyodhihirisha ushindani wa soko na ongezeko la uhitaji wa maudhui yake.
Anajivunia kile anachokifanya na anasema yuko huru nalo kwa sababu kinamsaidia kulipa gharama zake za maisha.

Hata hivyo, taaluma yake haijakosa utata. Video za faragha zilizovuja, hasa ile iliyopewa jina la “waterfall”, zilisababisha maoni mseto na mjadala mkubwa miongoni mwa umma. Video hiyo iliwavutia Wakenya wengi kutaka kumjua zaidi.
Wengi walikosoa maudhui yake, hasa kwa sababu yanahusiana na watu wazima, lakini Alicia hajawahi kuaibika kwa hilo.
Kwa kweli, hucheka na kufanya mzaha wa hali hiyo wakati mashabiki wake wanapomkosoa.
Maafisa wa serikali walikemea hadharani maudhui hayo, wakionya kuwa huenda yalikiuka viwango vya kisheria na maadili ya kijamii.
Hadi sasa, Alicia hajatoa taarifa yoyote kuhusu hali yake ya mahusiano.
Maoni ya umma kumhusu Alicia yamegawanyika. Wapo wanaomsifu kwa ujasiri wake na uhuru wa kifedha, huku wengine wakitilia shaka athari za kiutamaduni na kimaadili za kazi yake.