DAR-ES-SALAAM, JULAI 31, 2025 — Msanii wa Bongo Flava Zuchu amewajia juu wanaompigia Diamond Platnumz simu nyakati za usiku wa manane, akidai wanavunja heshima ya ndoa yao.
Zuhura Othman ameibuka hadharani na kulaani tabia ya baadhi ya watu kumpigia mumewe, Diamond Platnumz, simu usiku wa manane, akisema jambo hilo linakiuka mipaka ya heshima ya ndoa.
Tahadhari ya Hadharani Instagram
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mnamo Alhamisi, Julai 31, 2025, Zuchu alisema kuwa kuna mtu anayempigia Diamond simu usiku, licha ya kujua kuwa ana mke. Aliashiria kuwa mtu huyo anaanza jina lake kwa herufi “A”.
“SieIewi mtu anawezaje kumpigia mume wa mtu usiku wa manane, tena usiku sana… Hujui ana mke?”
“Kama unajua jina lako linaanza na A, naona simu zako. Acha kumpigia mume wangu.”
Diamond Athibitisha Ndoa kwa Mafumbo
Mnamo Jumapili, Juni 1, 2025, Diamond Platnumz alitangaza kufunga ndoa na Zuchu kupitia Instagram kwa kupakia picha zao wakiwa wamevaa mavazi ya harusi ya Kiislamu. Alifuatisha na ujumbe wa mafumbo kuhusu ukomavu na subira.
“Mmoja ya vitu ambavyo nimejifunza ni ukomavu wa kukaa kimya… Ukimya huu unahitaji kiwango kikubwa cha subira. Unahitaji uvumilivu hasa pale ambapo mtu au watu wanakusingizia hadharani, huku ukijua ukweli lakini unachagua kunyamaza kimya.”
“Siyo rahisi, lakini thawabu zake ni kubwa kwa sababu mapambano yako hupiganwa na Mungu, na mwisho wa siku unashinda kila wakati.”
Aliendelea kusema kuwa amewahi kuoa hapo awali, lakini siku moja atafunguka kuhusu kilichotokea.
“Nafahamu kila mtu ana picha tofauti kuhusu Diamond Platnumz na ndoa. Lakini leo nataka niwaambie kuwa Diamond Platnumz amewahi kuoa… Na ipo siku nitawaeleza kilichotokea.”
Video Inayoonyesha Furaha ya Ndoa
Katika video moja inayosambaa mitandaoni, Zuchu anaonekana akiwa ndani ya gari pamoja na Diamond, huku akiwa na furaha akisema:
“Mume wangu, tumeoa.”
Diamond ambaye alikuwa pembeni, alicheka kwa bashasha, akiashiria furaha na ridhaa yake kuhusu ndoa hiyo.
Mama Dangote Athibitisha
Mama mzazi wa Diamond, maarufu kama Mama Dangote, pia alithibitisha ndoa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
“Alhamdulillah imekwenda salama. Hongera mwanangu Naseeb na mkeo Zuhura.”
Mashabiki Watoa Maoni
Katika mitandao ya kijamii, mashabiki walitoa maoni mbalimbali. Wengine walimsifia Zuchu kwa ujasiri wake wa kumlinda mume wake, huku wengine wakihisi kuwa masuala ya kifamilia hayapaswi kuwekwa hadharani.
Mmoja aliandika: “Zuchu ana haki ya kumlinda mume wake. Watu wajue mipaka.”
Mwingine akaandika: “Mambo ya ndani ya ndoa hayawekwi mitandaoni kila saa. Vitu vya faragha vinahitaji hekima.”