logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Anajua ukichaa wangu" Harmonize kumtuza mwanadada kwa gari na nyumba

Amesema anapanga kutimiza hadi yake kwa Zuwena kabla ya mwezi wa Mei kuisha.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri07 May 2022 - 11:52

Muhtasari


•Harmonize amefichua kuwa Zuwena ndiye kijakazi wake wa kwanza huku akidai kuwa sio kijakazi wake tu bali pia ni kama dada yake.

•Konde Boy ametangaza kuwa anapanga kutimiza hadi yake kwa Zuwena kabla ya mwezi wa Mei kuisha.

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize ameahidi kumzawadi mjakazi wake Zuwena kwa nyumba na gari.

Amepiga hatua hiyo kama ishara ya shukran kwa huduma alizomtolea katika kipindi cha miaka saba ambacho kimepita.

Konde Boy ametangaza kuwa anapanga kutimiza hadi yake kwa Zuwena kabla ya mwezi wa Mei kuisha.

"Ni kama shangazi yangu. Miaka 7 anajua nakula nini. Ananipikia, ananifulia, ananifanyia usafi, anajua ukichaa wangu wote. Kabla ya Juni namnunulia gari lake la kwanza na kinyumba hata cha chumba 3 mkoani kwao," Harmonize alitangaza kupitia Instagram.

Harmonize amefichua kuwa Zuwena ndiye mjakazi wake wa kwanza huku akidai kuwa sio kijakazi wake tu bali pia ni kama dada yake.

Amemshukuru sana mwanadada huyo kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akifanya na kumtakia baraka za Maulana.

"Mungu akubariki dada Zuuh maana si kwa vipipi vya sigara ambavyo unavifagia kila siku kwenye mashuka majivu vipi," Aliandika.

Mwanamuziki huyo aliambatanisha ujumbe wake kwa video ya Zuwena akiwa jikoni akipakua chakula.

Siku za hivi majuzi Harmonize amekuwa akiwanunulia watu wa karibu naye magari kwa sababu tofauti.

Tayari amemnunulia magari mawili aliyekuwa mpenzi wake Kajala Masanja akiwa na nia ya kuomba msamaha na kurejesha mahusiano ya.

Mapema wiki hii alimnunulia mama yake mzazi gari aina ya Harrier na kufichua kuwa hiyo ndiyo gari aipendayo zaidi.

Mwezi uliopita alimnunulia gari ndogo mpiga picha wake Jabulant.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved